Alhamisi, 10 Aprili 2014
Jumatano, 9 Aprili 2014
MVUA YAKWAMISHA MCHEZO WA AZAM NA RUVU SHOOTING.
Mchezo wa mpira wa miguu ligi kuu ya Tanzania kati ya AZAM na RUVU SHOOTING uliokuwa ufanyike katika uwanja wa mabatini umeahilishwa kutokana na uwanja kujaa maji, mchezo huo sasa unatarajiwa kufanyika kesho.(Hudugu Ng'amilo)
Jumatatu, 7 Aprili 2014
Jumamosi, 5 Aprili 2014
RICHARD MAVOCAL/ROHO YANGU OFFICIAL VIDEO HD 720.
Rich Mavoko alianza kutoa vipande vya video hii muda mrefu sana kwenye account yake ya instagram lakini baada ya muda wote huo hatimaye ameitoa video nzima.
Story kubwa ya hii video ilikua ni Rich Mavoko kukodisha camera ya gharama kutoka Kenya na kwa ajili ya ku-shoot video hii.
Alhamisi, 3 Aprili 2014
Jumanne, 1 Aprili 2014
Jumamosi, 29 Machi 2014
Alhamisi, 27 Machi 2014
RAIS JAKAYA KIKWETE AONGEA NA WANANCHI WILAYANI MUHEZA, AHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA TANGA
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mtoto Hassan Mustafa(13) mwenye tatizo la kudumaa muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukagua na kuzindua maabara katika shule ya sekondari ya Potwe, wilayani Muheza
MWILI WA MAREHEMU MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA WAWASILI DODOMA LEO
Askari wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Dodoma leo Machi 27, 2014. Marehemu ataagwa kwenye viwanja vya Nyerere Dodoma Machi 28, 2014 kabla ya kusafirishwa kwenda kilosa kwa mazishi.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Jumatano, 26 Machi 2014
Jumanne, 25 Machi 2014
Jumatatu, 24 Machi 2014
Jumapili, 23 Machi 2014
Jumamosi, 22 Machi 2014
Jumatano, 19 Machi 2014
Jumanne, 18 Machi 2014
Jumapili, 16 Machi 2014
Jumamosi, 15 Machi 2014
Ijumaa, 14 Machi 2014
Alhamisi, 13 Machi 2014
NDEGE WA AJABU WAIKUMBA BUKOBA, KINYESI CHAO CHAUA KUKU 516, NA MBUZI 12...!!!!!
Ndege wa ajabu wakiwa juu ya miti katika Kisiwa cha Musira kilichopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Ndege hao wamezua hofu kwa wakazi kutokana na kinyesii chao kudhuru mifugo na ndege.
Jumatano, 12 Machi 2014
Jumatatu, 10 Machi 2014
Jumapili, 9 Machi 2014
Jumamosi, 8 Machi 2014
Ijumaa, 7 Machi 2014
ADHA YA MVUA KUBWA JIJINI DAR ES SALAAM
Dereva wa Bodaboda, akiwa na abiria wake, wakinyanyua miguu kukwepa kulowa na maji ya mvua yaliyofurika kwenye barabara ya Mbozi, Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana. Mvua ya siku mbili tu tayari imeanza kuletakasheshe, si kwa wenye magari pia wenye bodaboda, watembea kwa miguu.
BIBI MJASIRIAMALI WA MAKOPO AENDESHA MAISHA DAR
Makopo yakiwa eneo la nyumba ya bibi huyo ambaye anaonekana kwa mbali akiondoka baada ya kuongea na paparazi wetu.
MZUNGU TAPELI ANASWA NA MAHELA KIBAO YA BANDIA HAPA BONGO
Kamanda Suleiman Kova
JAN ELOFF AKITOLEWA NJE YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM
JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY
Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.
Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyefahamika kwa jina la JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar.
Taarifa zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU, pamoja na Kutoa Euro Feki.
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukamatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.Kufuatia kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi 'kupigwa' na mzungu huyo basi wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.
Alhamisi, 6 Machi 2014
Jumatano, 5 Machi 2014
RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.
Akizungumza katika kikao maalum na Maafisa Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.
Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda.
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.
Katika ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
.jpg)








.jpg)
.jpg)







.jpg)































