Jumatano, 19 Februari 2014
TAZAMA JINSI MWANAMKE HUYU YALIYOMPATA BAADA YAKUTAKA KUONGEZA UKUBWA WA MAKALIO YAKE
UKRAINE INAWAKA MOTOOOOOOO...!!!
Upinzani huko Ukrain umeapa kutotoka uwanja wa uhuru wanakoendeleza maandamano hayo.
Wakuu kutoka umoja wa Ulaya wameshtumu vikali rais wa Ukrain Viktor Yanukovych, kwa makabiliano makali baina ya polisi na waandamanaji yanayoingia siku ya pili sasa .
Waziiri Mkuu wa Poland , Donald Tusk, amesema atapendekeza Ukrain iwekewe vikwazo vya kiuchumi huku yule wa Sweden Carl Bildt akiongeza kuwa damu ya watu 25 waliokufa katika maandamano hayo iko mikononi mwa Yanukovych.
Vile vile wameutaka upinzani kuzuia machafuko zaidi ambayo yanasambaa kwengineko nchini humo.

IMANI ZA KISHIRIKINA ZAPELEKEA NYUMBA ISHIRINI KUCHOMWA MOTO GEITA
Wananchi wenye hasira kali wameteketeza kwa moto zaidi ya nyumba ishirini na kuvunja nyingine katika kijiji cha Kilombero mkoani Geita kutokana na mauaji ya watu watano yaliyotekelezwa kwa nyakati tofauti kwa kukatwa mapanga. Tukio la Februari 6 la mwanamke Felista Mathias kuuawa kwa mapanga limewachochea zaidi wananchi hao kuvamia nyumba za wanaodaiwa kuhusika februari 17 wakati ukoo ya Kisumo ukitajwa kuhusika na mauaji yanayotokea kijijini humo ambapo mmoja wao Elias Kisumo amekamatwa. Kumekuwa na matukio ya mauaji ya mapanga kwa wazee katika kijiji hiki, na matukio hayo yanahusisha ushirikina, uvamizi wa mifugo katika mashamba ya watu na hata visasi. kuuwawa kwa mwanamke FELISTA MATHIAS mwenye umri wa miaka 55 sababu kubwa...
WAZIRI MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MABWEPANDE
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za Serikali zipatazo 851 zilizopo katika eneo la Mabwepande, Kinondoni,jijini Dar es Salaam zinazosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Huu ni muendelezo na mikakati ya Wizara ya Ujenzi ya kuwajengea na kuwauzia watumishi wa Serikali nyumba kwa bei nafuu.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka Bw. Mwakalinga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Magufuli akiendelea na ukaguzi wa Ujenzi huo.
Hizi ni baadhi ya sehemu ya nyumba hizo.

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)