promotion

Jumanne, 6 Mei 2014

RAY C HOI KITANDANI HOSPITALI YA MWANANYAMALA KWA "GONJWA" HATARI LILILOZUKA JIJINI DAR


















FAHAMU UGONJWA WA KISONONO, DALILI NA TIBA YAKE.











Sababu za kukojoa mara kwa mara

Wanaume,hasa wenye umri mkubwa husumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya ‘prostate’ (tezi kibofu ya mamalia dume). Ni tezi iliyo kwenye viungo vya uzazi vya wanaume kilicho chini ya kibofu panapopitia mrija wa mkojo.Kazi ya ‘prostate’ ni kudhibiti kibofu na mtiririko wa mkojo.

Pia ni muhimu katika tendo la ndoa kwani humwezesha mwanamume kuwa na nguvu ya kufikia kilele. Inatoa asilimia 95 ya ute unaosafirisha mbegu za kiume kwani ina nguvu ya kusukuma ute ulio na mbegu ili upite kwenye mrija wa kukojolea na kutoa mbegu n-nje.‘Prostate’ ya kawaida kwa mwanamume mtu mzima ina ukubwa kama punje ya karanga na ukubwa huu huongezeka kadiri mtu anavyokua,

hasa pale anapofikisha umri wa miaka 40 na kuendelea. Katika umri wa miaka 40 tezi huanza kutanuka na kadiri inavyotanuka, hubana mrija wa kupitisha mkojo na kufanya mkojo utoke kwa shida na kusababisha tatizo katika tendo la ndoa.
Dalili za mwanzo ni kwenda haja ndogo mara kwa mara, hasa usiku; haja ndogo isiyoweza kudhibitiwa na mara nyingi mtu huweza kujikojolea. Pia mkojo hutoka kwa udhaifu ama kwa kukatika katika, kupata shida wakati wa kukojoa wakati wa kuanza au kumaliza.

Wakati mwingine mwanamume hupata maumivu wakati wa kukojoa na hata kutoka damu. Maumivu huenea kwenye sehemu za mgongo, kiuno na sehemu za juu ya mapaja na kupunguza uwezo wa tendo la ndoa au kupata maumivu wakati wa kufikia kilele. Pia kutokuwa na amani au kuhangaika wakati wa tendo la ndoa.

Matatizo mengine ni kupata maambukizi ya magonjwa kwenye kibofu, njia ya mkojo na figo. Kwa hiyo mkojo hubaki kwenye damu na kuwa sumu. Utafiti waonesha kuwa asilimia 50 ya wanaume wa umri kati ya 50 na 70 wana shida ya kutanuka tezi la ‘prostate’. Asilimia 25 ya wanaume wenye umri wa miaka 30 wana chembechembe za ‘prostate cancer’.

‘Prostate cancer’ ndio aina kuu ya ‘cancer’ (saratani) inayowashambulia sana wanaume na yaweza kuwa hafifu, inayotibika au kumdhuru mtu na kumwua.

‘Fibroid’ ni kitu gani? Ni uvimbe katika sehemu za uzazi (uterus) wa mwanamke ambazo hutengenezwa na kambakamba zilizofungamana (muscle fibre). ‘Fibroid’ huanza kwa ukubwa kama punje ya njegere lakini huweza kukua kwa ukubwa wa tikitimaji.

Inakadiriwa kuwa asilimia 20 na 50 ya wanawake wana tatizo hili au huwa nalo katika kipindi fulani cha maisha yao. ‘Fibroids’ hupatikana zaidi kwa wanawake wa umri kati ya miaka 30 na 40 na hupungua ukubwa mara tu wanapoingia katika umri wa utu uzima.

Uchunguzi uliofanywa kule Marekani waonesha kuwa ‘fibroids’ huwapata wanawake wa kiafrika mara tisa zaidi ya wanawake wa kizungu. Ingawa sababu au chanzo hasa cha ‘fibroids’ hakijulikani, utafiti waonesha kuwa huchochewa na ‘oestrogen’ mwilini.

Mara nyingi ‘fibroids’ hukua kwa mwanamke pale kiwango cha ‘oestrogen’ kinapoongezeka mwilini na pia ‘fibroids’ hupungua wakati kiwango cha ‘oestrogen’ nacho kikipungua.

‘Oestrogen’ ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia. Mfano ni ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi. Pia wanawake wenye uzito wa zaidi ya kilo 70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata ‘fibroids’ kutokana na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ katika umri huo.

Zamani ‘fibroids’ ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa sababu vidonge hivyo vilikuwa na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen.’ Hivi sasa vidonge hivi vya uzazi wa mpango havina kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ kama ilivyokuwa zamani.

‘Fibroids’ zinatofautishwa kutokana na sehemu ilipotokea. Yapo makundi mawili yanayoweza kugawanya aina za ‘fibroids.’ Zinazotokea ndani ya mji wa mimba na zinazotokea kwenye kuta za n-nje ya mji wa mimba.

Yakadiriwa kuwa asilimia 75 ya wanawake wenye ‘fibroids’ hawana dalili zozote na wala hawajui kama wana ‘fibroids.’ Utambuzi wa dalili za ‘fibroids’ hutegemea ukubwa wake na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia huchangiwa na dalili anazopata mtu.
Mfano: ‘fibroid’ ndogo iliyo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na ‘fibroid’ kubwa inayoota n-nje ya kizazi.

Dalili kubwa inayofahamika zaidi ni ile ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi. Dalili nyingine ni maumivu ya tumbo. Pia huathiri mfumo wa haja ndogo na kubwa, kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogo kidogo, kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo, kutopata mimba na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

‘Fibroids’ zaweza kusababisha matatizo kama kuharibu mimba au mwanamke kutoshika mimba kutokana na mirija ya uzazi kubanwa au msukumo unaosababishwa na ‘fibroids’, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus).

Mwanamke anapokuwa mjamzito na pia akawa na ‘fibroids’, wakati huo mwili huweza kusitisha kupeleka damu kwenye ‘fibroids’ na kuifanya isinyae. Kama hili likitokea, husababisha maumivu makali ya tumbo na kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa na baadaye mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.

Wakati wa kujifungua, kama ‘fibroid’ itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka au ikishindikana, mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliye tumboni.

Utawezaje kugundua kama una ‘fibroids’? Kama hakuna dalili yawezekana tu kwa kufanya vipimo. Dalili zikiwapo na kuhisi unalo tatizo la ‘fibroids’, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo kujua kama una ‘fibroids’ au la.
Daktari atafanya vipimo vya ‘Ultrasound’ (mionzi), ‘Hysteroscopy’ (kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke) na ‘Laparosopy’ (upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke).

Njia iliyozoeleka ya kuishi na ‘fibroids’ zinazotoa damu nyingi ni kuzilinda na si kuzitibu (monitor rather than treat them). Utashauriwa kupata uangalizi/uchunguzi wa mara kwa mara ingawa bado utahitaji kupata msaada zaidi kwa jinsi unavyojisikia.

Kuna njia kuu mbili za kutibu ‘fibroids’. Kutumia dawa (drug treatment). Mkusanyiko wa dawa zijulikanzo kama ‘GnRH analogues’ hupunguza kiwango cha ‘oestrogen’ mwilini na hivyo kusababisha ‘fibroid’ kusinyaa. Uchunguzi waonesha kuwa dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa ‘fibroid’ kwa aslimia 50. Pia dawa hizi hupunguza mzunguko wa hedhi.

Yashauriwa kwamba matumizi ya dawa za ‘GnRH analogues’ yasizidi miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa baadaye. Pia mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi, wiki chache baadaye ‘fibroids’ huanza kukua tena na mwanamke huanza kupata hedhi kama awali lakini ikiambatana na maumivu makali. Baadhi ya wanawake huwa hawapati hedhi tena kwa maisha yao yote.

Upasuaji unahusisha mambo yafuatayo: Kuiondoa ‘fibroid’ yenyewe na kuacha kizazi (myomectomy); kukiondoa kizazi kabisa (hysterectomy), kuzuia damu kwenda kwenye ‘fibroids’ (uterine artery embolisation). Pia iko njia isiyozoeleka sana ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni zikielekea zilipo ‘fibroids’ kwa ajili ya kuziua kwa kemikali maalumu.

Makala haya yameandaliwa kwa msaada wa jarida la Forever Living Products.
marobarnabas@yahoo.com