Maisha ya Ommy Dimpoz kwenye script ya video yake mpya aliyoishoot hivi karibuni nchini Uingereza yanaonekana yalikuwa magumu sana.
Tayari staa huyo wa Tupogo ameshawaonesha mashabiki wake baadhi ya picha za uchukuaji wa video hiyo iliyoongozwa na Mnaijeria aishiye London, Uingereza, Moe Musa zikiwemo zile anazoonekana akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Muongozaji huyo wa video leo ameshare picha nyingine inayoonesha akiwa kwenye mchakato wa kuhariri video hiyo na tumegundua kitu kingine- Ommy alikufa kwenye video hiyo.. patamu hapo (kwa sauti ya Soudy Brown).
Katika picha hiyo, Ommy Dimpoz anaonekana akiwa kwenye jeneza. “Color Grading/Correcting @ommydimpoz Music Video. Visuals look #Frosh2Death,” ameandika muongozaji huyo.
Hivi karibuni, Ommy Dimpoz alisema kabla hata ya kufahamu kuwa Sofia Skvortsova ndiye model atakayemtumia kwenye video yake, alikuwa amemuona na akatamani msichana kama yeye aonekane kwenye video hiyo.
“Kwanza yule msichana wakati mimi natoka naelekea location, tupo kwenye taa hivi ambapo tunavuka taa ambazo ukizivuka unaelekea eneo la location nikawa namuona msichana yaani mzuri halafu nikawa nasema kimoyomoyo kwasababu nilikuwa sijamuona nikakutana naye location moja kwa moja, hatukukutana siku ya kwanza tukapanda, hapana, alikuja moja kwa moja siku ya kushoot,” Ommy aliiambia Bongo5.
Alisema baada ya kumuona Sofia alimwambia mshkaji wake kuwa anatamani msichana kama huyo awe kwenye video yake. Ameongeza kuwa siku ya kufanya video alipofika location akamkuta Sofia eneo hilo na kumchanganya zaidi Ommy.
“Baadaye Moe Musa ndio ananiita ananitambulisha ‘huyu ndio video model, sijui unamuonaje,” ameelezea Ommy. “Mimi nikamwambia, ‘mimi nimempenda sana’ mimi nilimuambia nataka msichana mzuri kulingana na uzuri wa nyimbo na maadhui ya nyimbo yalihitaji msichana mzuri.”
Ommy alida kuwa kama mambo yakienda sawa anafikiria kumleta Sofia Tanzania siku ya uzinduzi wa video hiyo. Tangu amtambulishe kwenye Instagram, Sofia amepata followers wengi kutoka Tanzania. “Alipata followers wengi kutoka huku kwahiyo akashangaa sana halafu akaappreciate.”
By mcharoman
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni