Ofisa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (kulia) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MIC Tanzania (Tigo), Cecilia Tiano (kushoto) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya miradi miwili ya upelekaji mawasiliano vijijini awamu ya 2A kati ya Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF)na kampuni za simu za mkononi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Miradi hiyo ni upelekaji wa mawasiliano mipakani na maeneo maalum na mradi wa kuunganisha Intaneti kwenye Shule za Umma. |