Makopo yakiwa eneo la nyumba ya bibi huyo ambaye anaonekana kwa mbali akiondoka baada ya kuongea na paparazi wetu.
Harakati za ujasiriamali za bibi mmoja maeneo ya Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako anakusanya makopo na kuyauza kwa ajili ya kuendesha maisha yake kiufasaha zaidi bila ya kubugudhiwa, kama alivyosema.
Akiongea na mtandao huu mfanyabiashara huyo aligoma kutaja jina lake huku akitoa sharti la kutokupigwa picha lakini alisema biashara hiyo ya makopo imemfanya aendeshe maisha bila ya wasiwasi wowote na pia anamudu kuwasomesha wajukuu zake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni