Alhamisi, 20 Februari 2014
MAMA WA MAKAMO AGARAGARA HADHARANI BAADA YA KUTAPELIWA T.SH MILIONI 5.4 MJINI MOSHI LEO
MATAPELI HAO WALIUTUMIA MGAHAWA WA FRESH COACH KUTAPELI..!
Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20.
Mama akilia kwa uchungu.. Keleuwieeeeeee...!!!!!
Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20.
Mama akilia kwa uchungu.. Keleuwieeeeeee...!!!!!
KANISA LAHIMIZA WAUMINI WAKE KWENDA IBADANI WAKIWA UCHI
KANISA moja nchini Amerika limewaruhusu waumini wake kuhudhuria ibada kanisani huku wakiwa uchi.
Waumini wa kanisa hilo lililoko kusini mwa jimbo la Virginia, sasa wanalazimika kuvua nguo zao pindi tu wanapoingia ndani ya jumba la ibada.
Akihutubia wanahabari, kasisi wa kanisa hilo, Bw Allen Parker, alisema walifikia uamuzi huo wa kuomba uchi baada ya kubainisha kuwa mavazi yana 'udanganyifu fulani’ na akaongezea kwamba hatua hiyo 'itawafanya waumini wote kuwa sawa bila kuwepo kwa utofauti wa kimapato’.
Kasisi huyo alisema hatua hiyo ina ithibati ndani ya Biblia huku akidai kuwa miujiza mingi katika Biblia ilitendeka wakati ambapo wahusika walikuwa uchi. Kwa mfano, alisema Yesu Kristo alikuwa uchi aliposulubishwa msalabani na wakati alifufuka kutoka kaburini.
J
apo matakwa ya kuwa uchi ndani ya kanisa si lazima, wengi wa waumini wanaonekana kuitikia wito huo. Baadhi ya waumini ambao hawapendi kusalia uchi wa mnyama kanisani wanavalia nguo za ndani.
Ambao wamekumbatia wito huo wanasema wamezoea kuwa uchi kanisani japo walikuwa wakiona haya siku za mwanzoni.
Pasta wa kanisa hilo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha runinga nchini humo, alisema anafuata nyayo za Yesu.
“Wakati ambapo Yesu alipitia hatua muhimu maishani alikuwa uchi,” akadai Bw Parker. “Alipozaliwa alikuwa uchi, aliposulubishwa alikuwa uchi na wakati ambapo alifufuka aliacha mavazi yake ndani ya kaburi. Ikiwa Mungu alituumba hivyo, Je, kuna hatia gani kuwa uchi kanisani?” akasaili.
Baridi
Mamia ya waumini wamekuwa wakivumilia baridi ya msimu wa baridi kali kila siku ya Jumapili kusikiliza Injili huku wakiwa uchi wa mnyama.
Wakati huo huo, maelfu ya watu wamekuwa wakifurika kwenye kanisa hilo kupiga picha. Zaidi ya watu 10,000 huzuru kanisa hilo kila mwaka.
“Waumini wanapata fursa ya kusikiliza na kujadili Neno la Mungu,” akasema msimamizi wa kanisa hilo huku akiongezea kuwa kuna baadhi ya watu ambao wana mali nyingi huku wengine hawana kitu chochote.
Alieleza kuwa wanapoomba wakiwa uchi tajiri na maskini huwa sawa mbele ya Mungu.
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE ATINGA MAHAKAMANI
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi hapo jana ametolea ushahidi mbele ya mahakama ya Wilaya ya Njombe dhidi ya kesi ya manunuzi hewa wa magurudumu matano na betri mbili za gari vyoti vikiwa na thamani ya shilingi milioni 14 inayomkabili aliyekuwa kaimu katibutawala wa wilaya hiyo ya wanging'ombe bw Eegray keiya.Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo , mkuu huyo wa Wilaya ya Wanging'ombe ambaye ni shahidi namba moja ameiambia mahakama kuwa ofisi yake pamoja na aliyekuwa akikaimu ofisi ya katibu tawalaWilaya ya Wanging'ombe waliagiziwa magurudumu tano aina ya gunrubk wa ajili ya gari yake lakini hakuwahi kuyaona magurudumu hayokatika ofisi yake."Kwa kipindi kile yanaletwa...
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)