Jumapili, 7 Desemba 2014
Raia wa Marekani na A.Kusini wauawa
Raia wa marekani Luke Somers na mwenzak wa Afrika kusini Pierre Korkie wameuawa na wapiganaji wa kundi la Alqaeda nchini Yemen |
Peresheni ya kuwaokoa iliongozwa na vikosi maaulum vya Marekani na Yemen katika jimbo la kusini la Shabwa.
Rais wa Marekani Barack Obama alilaani kile alichokieleza "mauaji ya kinyama" ya mateka hao wawili.
Walikua wanazuiliwa na wapiganaji wa kundi la al-Qaeda katika Bara arabu ambalo Marekani inalichukulia kuwa mojawapo wa matawi hatari duniani ya kundi kuu la al-Qaeda.
Kundi hilo lina makao yake Mashariki ya Yemen na limeweza kupata wafuasi wengi katika nchi masikini iliokumbwa na machafuko tangu kupinduliwa kwa Rais Ali Abdullah Saleh in 2011.
Maofisa wa ngazi za juu nchini marekani wameiambia BBC kua vikosi maalum vilivyoshiriki katika jitihada za kumuokoa Luke Somera nchini hawakuwa wanafahamu kuhusu mateka mwingine aliyekuwa akishikilwa na wanamgambo hao.
Shirika ambalo mwalimu huyo raia wa Afrika Kusini Pierre Korkie alikuwa akilifanyia kazi lilisema kuwa mateka huyo angeachiliwa leo jumapili kufuatia maafikiano ya kulipa fidia.
Marekani iliamrisha kuchukuliwa jitihada hizo kwa kuwa iliamini kwamba maisha ya bwana Somers yalikuwa hatarini.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)