promotion

Jumatano, 5 Machi 2014

Picha/Video: Chatu mwenye futi 10 alivyommeza mamba mzima mzima, walipigana kwa saa 5


























RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao maalum na Maafisa Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.

Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda. 
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.


Katika ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile. 
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT



























Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.

Magazeti ya leo March 05 2014


































MTOTO AUNGUZWA MIKONO YOTE MIWILI KWA KUDOKOA NJEGERE JIKONI P


njegere
Mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Jangwani, Manispaa ya Sumbawanga  amechomwa moto mikono  yake miwili, kutokana na tuhuma za kudokoa  njegere  zilizokuwa  zikichemka jikoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda amethibitisha mkasa huo  aliouita ni wa kikatili huku akimtaja  mtuhumiwa  kuwa ni Anifa  Lunyerere (18), mkazi wa Kitongoji  cha Bangwe, Manispaa ya Sumbawanga.

Kamanda Mwaruanda alisema Lunyerere alimchoma mikono mtoto huyo (jina limehifadhiwa) wiki iliyopita katika kitongoji  hicho cha Bangwe  saa  sita mchana.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, mtoto huyo alipohojiwa alidai alifikia uamuzi huo wa kudokoa njegere  baada ya kuzidiwa na njaa,  kwani alikuwa ametoka shuleni  ambako alikuwa hajala chochote.
"Mtoto  huyu alieleza  kuwa  wifi yake  huyo  amekuwa na  tabia  ya kumfanyia  vitendo  vya kikatili mara kwa  mara kama vile kumng'ata mgongoni  hata kama  hajakosea kitu chochote," alidai Kamanda Mwaruanda. 

 Mtuhumiwa huyo anashikiliwa Polisi  kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani  wakati wowote baada ya uchunguzi  wa awali  wa shauri lake kukamilika.