promotion

Jumapili, 9 Machi 2014

WATANZANIA WATATU NA WANYARWANDA WATATU WAKAMATWA KATIKA JARIBIO LA MAUAJI YA MKUU WA MAJESHI YA RWANDA


























Watanzania watatu ni miongoni mwa washtakiwa sita  wanaodaiwa kumvamia Mkuu wa Majeshi wa Rwanda  aliye mafichoni , Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa.
 
Washtakiwa hao  pamoja na Wanyarwanda watatu wamefikishwa katika mahakama za Afrika Kusini kujibu mashtaka hayo.
 
Jenerali Nyamwasa  alishambuliwa wiki hii, ikiwa ni muda mfupi baada ya mauaji ya Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Rwanda na mpinzani wa Rais Paul Kagame , Patrick Karegeya.
 
Ofisa usalama huyo aliuawa kwenye hoteli ya kifahari  mwanzoni mwa mwaka huu nchini Afrika ya Kusini.
 
Watanzania hao wanatuhumiwa kuhusika na mkasa wa  Jumatatu wiki hii   uliohusisha watu wenye silaha kuingia nyumbani kwa  Mkuu wa Majeshi wa zamani wa Rwanda, Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
 
Hata hivyo, Nyamwasa ambaye pia alinusurika  kifo mwaka 2010, hakuwapo nyumbani siku hiyo na hivyo kupona tena.
 
Mwanzoni mwa  mwaka huu, Karegeya aliyekimbilia Afrika Kusini mwaka  2007 baada ya kudaiwa kuwa alipanga mapinduzi ya kumng’oa Kagame madarakani akishirikiana   na  Jenerali Nyamwasa, aliuawa hotelini alipokuwa anaishi.
 
Wakosoaji wa Rais Kagame  wamemtuhumu kuhusika na mauaji ya Karegeya na mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanyika  nyumbani kwa Jenerali Nyamwasa.
 
Majina ya Watanzania hao hayakutajwa na haikufahamika  walishirikije katika mashambulizi hayo.
 

Taarifa hii ni kwa mujibu wa kituo cha  televisheni cha Al Jazeera iliyorushwa jana.
 

Hakuna maoni: