promotion

Ijumaa, 18 Aprili 2014

SABABU YA MAALIM GURUMO KUPOTEZA JICHO LAKE MOJA HII HAPA
























WAKATI Saluti5 ilipofanya ziara ya kwenda Masaki kijijini kwa mwimbaji Muhidin Maalim Gurumo aliyefriki Jumapili, ilipata mambo mengi mahsusi kutoka mwa gwiji huyo.

Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau  au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.
Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.
Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.
“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.
“Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.
“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akisimulia namna alivyopoteza jicho lake.

CHANZO: Saluti5.com






BREAKING NEWS: MELI YAZAMA ZIWA VICTORIA HIVI PUNDE





















Ni mwaka mmoja tangu Bi Kidude afariki dunia








Jumatano, 16 Aprili 2014

Jumamosi, 5 Aprili 2014

RICHARD MAVOCAL/ROHO YANGU OFFICIAL VIDEO HD 720.





Rich Mavoko alianza kutoa vipande vya video hii muda mrefu sana kwenye account yake ya instagram lakini baada ya muda wote huo hatimaye ameitoa video nzima.


Story kubwa ya hii video ilikua ni Rich Mavoko kukodisha camera ya gharama kutoka Kenya na kwa ajili ya ku-shoot video hii.





Alhamisi, 27 Machi 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGEA NA WANANCHI WILAYANI MUHEZA, AHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA TANGA



































Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mtoto Hassan Mustafa(13) mwenye tatizo la kudumaa muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukagua na kuzindua maabara katika shule ya sekondari ya Potwe, wilayani Muheza





MWILI WA MAREHEMU MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA WAWASILI DODOMA LEO



























Askari wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Dodoma leo Machi 27, 2014. Marehemu ataagwa kwenye viwanja vya Nyerere Dodoma Machi 28, 2014 kabla ya kusafirishwa  kwenda kilosa kwa mazishi. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.