promotion

Alhamisi, 12 Juni 2014

Diamond Platnumz akiwa na Mama yake mzazi wakicheza KITORONDO...


Kuna wengi watakuwa wameshaisikia hit mpya ya Diamond Platnumz ambayo ilivuja, hit hiyo inaitwa KITORONDO , Ngoma hii aijatoka bado ipo jikoni bado au labda Diamond mwenyewe ajaamua kuiachia rasmi ngoma hii amabayo kwa uchunguzi wangu tu nimegundua kuwa watu wengi wanaipenda nyimbo hii inagawa bado aijatoka rasmi.


































MSIKILIZE DIAMOND PLATNUM ALICHOKISEMA BAADA YA KUKOSA TUZO ZA MTV AFRIKA MUSIK AWADR 2014


















































Jumamosi, 24 Mei 2014

UNYAMA WA KUTISHA: MGANGA WA KIENYEJI AMNYONGA MTOTO WA DARASA LA KWANZA, AMKATA MIKONO, SEHEMU ZA SIRI NA KUMZIKA CHINI YA KITANDA CHAKE

















Mganga Mujingwa John akiwa katika ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Kagera.picha ya kulia akionyesha jinsi alivyomkaba na kumnyonga mtoto mdogo pia kukata viungo vyake kisha kuchimba shimo chini ya kitanda chake na kuuzika mwili.Hivi sasa yuko chini ya ulinzi.


WAKATI jamii ya Watanzania ikipigwa butwaa na ukatili wa kutisha aliofanyiwa mtoto wa miaka minne kwa kufungiwa ndani ya boksi kwa miaka mitatu mjini Morogoro, ukatili mwingine wa kutisha dhidi ya watoto umeripotiwa mkoani Kagera.

Katika mkoa huo, mganga wa kienyeji ametiwa mbaroni, akituhumiwa kumuua kwa kumnyonga, kumkata mikono na kumzika katika nyumba yake.
Mganga huyo, Mujingwa John (20) amekiri mbele ya jeshi la polisi kuhusika na mauaji ya mtoto Fausta Geofrey (8), mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kitunga kata ya Muhutwe, wilayani Muleba.
Anatuhumiwa kwamba, alimkamata kwa nguvu akienda shule na wenzake, akamuua, kumkata mikono, nyama ya mgongo, masikio na sehemu za siri kwa lengo la kuibanika na kutengeneza 'uchawi’ wake, kisha akachimba shimo na kuzika mwili ndani ya nyumba.
Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, George Mayunga aliyesema mganga huyo alikamatwa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, ambapo alikutwa akibanika viungo alivyovikata kutoka kwa mtoto huyo.
Aidha, akiwa polisi, mganga huyo alipewa fursa ya kueleza kilichotokea mbele ya waandishi wa habari, ambapo alidai alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo, kutokana na hali ngumu ya umaskini inayomkabili.
Alisema baada ya kumkamata mtoto huyo, alimkaba shingo na kumvuta hadi katika nyumba aliyokuwa akiishi, akamnyonga hadi kufa na baada ya kufa, alimkata ngozi ya mgongoni, mikono akianzia na mkono wa kushoto aliodai una bahati, sehemu za siri na masikio.
“Nilimkamata mtoto na kumuua, maana niliona nikikamata mtu mzima atanizidi nguvu na kupiga kelele,” alidai.
Alidai kuwa, “Nilipomaliza kumuua nilichimba shimo chini ya kitanda changu nikamzika na kutandaza nyasi juu yake ili isigundulike kama eneo hilo kuna shimo".
Mganga huyo aliyejitambulisha kuwa ni Msukuma, alidai viungo hivyo ambavyo hadi polisi wanafika, alikuwa bado akivikausha, angevichanganya na dawa ambayo angewapatia wateja wake ili iwasaidie kufanikisha mambo yao, ikiwamo kupata bahati na utajiri na alitarajia kuuza kwa Sh 500 kwa kila ujazo wa kijiko kimoja cha dawa yake.
Alisema hiyo ni mara yake ya kwanza kufanya tukio la aina hiyo na kwamba alihamia Muleba mkoani Kagera miaka miwili iliyopita akitokea Nyanguge wilaya ya Magu mkoani Mwanza. Alisema alirithi uganga huo kutoka kwa babu yake mzaa mama na kuwa alianza uganga akiwa na umri wa miaka minane na hakuwahi kwenda shule.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bisole katika Kata hiyo wilayani Muleba, Khamis Hassan, akizungumzia tukio hilo baada ya mauaji hayo, alidai muuaji alimkata mtoto huyo mikono yake miwili kabla ya kumzika.
Hassan alisema kuwa tukio hilo ni la Mei 21 mwaka huu asubuhi katika kijiji hicho, wakati mtoto huyo akiwa na wenzake wakielekea shuleni, ambapo inadaiwa aliitwa na kukamatwa na mganga huyo, aliyetambulika kwa jina la Mujingwa John (20).
Alisema kuwa baada ya taarifa za mtoto huyo kutoonekana kuzagaa, wanakijiji walikusanyana na kuanza msako, ambapo walikamata kundi la watu waliokuwa wakiwahofia kuhusika, hasa vijana.
Alisema baada ya kuwakamata watu hao, waliwaweka sehemu moja na kuwaita wanafunzi waliokuwa na marehemu, ambapo walimtambua mganga huyo kuwa ndiye aliyemwita na kumkamata mtoto huyo.
Mtendaji huyo alidai baada ya mganga huyo kutambuliwa, wananchi na polisi waliofika eneo hilo, walikwenda naye hadi katika nyumba anayoishi na kumtaka awaonyeshe alipo mtoto huyo. Alidai baada ya kumbana, aliwaonesha sehemu alikomzika, ambapo walichukua jembe na kuanza kufukua mwili wa mtoto huyo, uliokuwa umezikwa ndani ya nyumba aliyoishi mganga huyo.
Alidai baada ya mganga huyo kumuua mtoto huyo, alimkata mikono yake miwili na kisha kuchimba shimo ndani ya nyumba, ambapo baada ya kumzika alifukia shimo akatandaza nyasi juu yake na kisha kuweka kitanda chenye godoro alilokuwa akilala.
Alisema kuwa alipohojiwa ili kujua nani kamtuma kutekeleza unyama huo, mganga huyo alidai ilitokana na yeye kuoteshwa na mizimu yake, iliyomtaka kumuua mtoto ili amkate viungo vyake kwa ajili ya kuchanganya na dawa.

Alisema mikono hiyo alitaka kuibanika kwenye moto ili aichanganye na dawa, ambayo angewapatia watu wanaohitaji kupata utajiri. Tukio hilo limekuja siku chache wakati Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, likiendelea na uchunguzi wa kilichotokea mpaka mtoto mmoja mkoani hapa , akateswa na mama mlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na miezi tisa, mpaka alipotimiza miaka minne. 


Acha mara moja

Kama na ww pia una imani za kishirikina acha haraka nikumkosea mungu

MCHAWI ADONDOKA BAADA YA KUCHOKA KURUKA KWA MUDA MREFU ANGANI

Jumapili, 18 Mei 2014

KIJANA AFIA KABURINI WAKATI AKIFUKUA KABURI ILI AIBE FUVU LA MAREHEMU, TAZAMA PICHA






















Maiti ya kijana huyo ikiwa imenasa kaburini.

Ommy Dimpoz - Ndagushima ( Official Video )

VIDEO MPYA YA WIMBO WA Ommy Dimpoz - Ndagushima ( Official Video ) IMETULIA SANAA HONGERA KIJANA







Video ya wimbo mpya wa Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’ ilitambulishwa jana jioni kwenye kituo cha TV cha MTV Base kwenye show yake ya Best of Spanking New. Na sasa itazame kwa mara ya kwanza hapa. Video hiyo ilifanyika jijini London na iliongozwa na Moe Musa.

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ADAMU PHILIP KUAMBIANA AMBAYE HATUMO NAE DUNIANI TENA


































 Marehemu Adam philp kuambiana enzi za uhai wake

Ijumaa, 9 Mei 2014

NEWS ALERT: WANAFUNZI 212 WA CHUO CHA POLISI MOSHI WAFUKUZWA BAADA YA KUBAINIKA WAMETUMIA VYETI BANDIA

Katika hali ya kushtukiza leo chuo cha mafunzo ya taaluma ya Jeshi la polisi Moshi, kimewafukuza mafunzoni jumla ya wanafunzi 212 wa uaskari, kutokana na sababu za kughushi vyeti vya elimu ya sekondari..

Hayo yamesemwa Leo na Mkuu wa Taaluma na Utumishi wa jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo ya taluma ya Polisi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Kamishna Andengenye amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), lilifanya uhakiki wa Vyeti vya wanafunzi wote 3,415 waliojiunga na mafunzo hayo Desemba mwaka jana ambapo waligundua kuwa wanafunzi 212 kati yao hawakuwa na sifa kutokana na sababu za kughushi vyeti.

"Katika kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa na askari wenye uweledi na uaminifu kwa raia na taifa kwa ujumla, tuliendelea na zoezi la kuhakiki vyeti kwa kushirikiana na baraza la mitihani la taifa, ambapo vyeti vya wanafunzi wa uaskari 212 kati ya walioripoti vimeonekana kuwa ni vya kughushi," amesema Andengenye.

Amesema kufuatia hali hiyo pamoja na kuwaachisha mafunzo wanafunzi hao 212, Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na taasisi nyingine linaendelea kufanya upelelezi ili kuhakikisha kuwa hatua za kisheriazinachukuliwa dhidi ya wanafunzi hao na maaskari wote watakaobanika kughushi vyeti.
 



By mcharoman;
                                    AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOGY HII KARIBU TENAE
 


MZEE ANAYEISHI WODINI KWA MIAKA 41 SASA, KUENDELEA KUSOTA WODINI KWA KUWA HANA NDUGU



























VIBAKA WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUSHUSHIWA KIPIGO NA WANANCHI KIJITONYAMA JIJINI DAR





















Jumanne, 6 Mei 2014

RAY C HOI KITANDANI HOSPITALI YA MWANANYAMALA KWA "GONJWA" HATARI LILILOZUKA JIJINI DAR


















FAHAMU UGONJWA WA KISONONO, DALILI NA TIBA YAKE.











Sababu za kukojoa mara kwa mara

Wanaume,hasa wenye umri mkubwa husumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya ‘prostate’ (tezi kibofu ya mamalia dume). Ni tezi iliyo kwenye viungo vya uzazi vya wanaume kilicho chini ya kibofu panapopitia mrija wa mkojo.Kazi ya ‘prostate’ ni kudhibiti kibofu na mtiririko wa mkojo.

Pia ni muhimu katika tendo la ndoa kwani humwezesha mwanamume kuwa na nguvu ya kufikia kilele. Inatoa asilimia 95 ya ute unaosafirisha mbegu za kiume kwani ina nguvu ya kusukuma ute ulio na mbegu ili upite kwenye mrija wa kukojolea na kutoa mbegu n-nje.‘Prostate’ ya kawaida kwa mwanamume mtu mzima ina ukubwa kama punje ya karanga na ukubwa huu huongezeka kadiri mtu anavyokua,

hasa pale anapofikisha umri wa miaka 40 na kuendelea. Katika umri wa miaka 40 tezi huanza kutanuka na kadiri inavyotanuka, hubana mrija wa kupitisha mkojo na kufanya mkojo utoke kwa shida na kusababisha tatizo katika tendo la ndoa.
Dalili za mwanzo ni kwenda haja ndogo mara kwa mara, hasa usiku; haja ndogo isiyoweza kudhibitiwa na mara nyingi mtu huweza kujikojolea. Pia mkojo hutoka kwa udhaifu ama kwa kukatika katika, kupata shida wakati wa kukojoa wakati wa kuanza au kumaliza.

Wakati mwingine mwanamume hupata maumivu wakati wa kukojoa na hata kutoka damu. Maumivu huenea kwenye sehemu za mgongo, kiuno na sehemu za juu ya mapaja na kupunguza uwezo wa tendo la ndoa au kupata maumivu wakati wa kufikia kilele. Pia kutokuwa na amani au kuhangaika wakati wa tendo la ndoa.

Matatizo mengine ni kupata maambukizi ya magonjwa kwenye kibofu, njia ya mkojo na figo. Kwa hiyo mkojo hubaki kwenye damu na kuwa sumu. Utafiti waonesha kuwa asilimia 50 ya wanaume wa umri kati ya 50 na 70 wana shida ya kutanuka tezi la ‘prostate’. Asilimia 25 ya wanaume wenye umri wa miaka 30 wana chembechembe za ‘prostate cancer’.

‘Prostate cancer’ ndio aina kuu ya ‘cancer’ (saratani) inayowashambulia sana wanaume na yaweza kuwa hafifu, inayotibika au kumdhuru mtu na kumwua.

‘Fibroid’ ni kitu gani? Ni uvimbe katika sehemu za uzazi (uterus) wa mwanamke ambazo hutengenezwa na kambakamba zilizofungamana (muscle fibre). ‘Fibroid’ huanza kwa ukubwa kama punje ya njegere lakini huweza kukua kwa ukubwa wa tikitimaji.

Inakadiriwa kuwa asilimia 20 na 50 ya wanawake wana tatizo hili au huwa nalo katika kipindi fulani cha maisha yao. ‘Fibroids’ hupatikana zaidi kwa wanawake wa umri kati ya miaka 30 na 40 na hupungua ukubwa mara tu wanapoingia katika umri wa utu uzima.

Uchunguzi uliofanywa kule Marekani waonesha kuwa ‘fibroids’ huwapata wanawake wa kiafrika mara tisa zaidi ya wanawake wa kizungu. Ingawa sababu au chanzo hasa cha ‘fibroids’ hakijulikani, utafiti waonesha kuwa huchochewa na ‘oestrogen’ mwilini.

Mara nyingi ‘fibroids’ hukua kwa mwanamke pale kiwango cha ‘oestrogen’ kinapoongezeka mwilini na pia ‘fibroids’ hupungua wakati kiwango cha ‘oestrogen’ nacho kikipungua.

‘Oestrogen’ ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia. Mfano ni ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi. Pia wanawake wenye uzito wa zaidi ya kilo 70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata ‘fibroids’ kutokana na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ katika umri huo.

Zamani ‘fibroids’ ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa sababu vidonge hivyo vilikuwa na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen.’ Hivi sasa vidonge hivi vya uzazi wa mpango havina kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ kama ilivyokuwa zamani.

‘Fibroids’ zinatofautishwa kutokana na sehemu ilipotokea. Yapo makundi mawili yanayoweza kugawanya aina za ‘fibroids.’ Zinazotokea ndani ya mji wa mimba na zinazotokea kwenye kuta za n-nje ya mji wa mimba.

Yakadiriwa kuwa asilimia 75 ya wanawake wenye ‘fibroids’ hawana dalili zozote na wala hawajui kama wana ‘fibroids.’ Utambuzi wa dalili za ‘fibroids’ hutegemea ukubwa wake na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia huchangiwa na dalili anazopata mtu.
Mfano: ‘fibroid’ ndogo iliyo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na ‘fibroid’ kubwa inayoota n-nje ya kizazi.

Dalili kubwa inayofahamika zaidi ni ile ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi. Dalili nyingine ni maumivu ya tumbo. Pia huathiri mfumo wa haja ndogo na kubwa, kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogo kidogo, kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo, kutopata mimba na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

‘Fibroids’ zaweza kusababisha matatizo kama kuharibu mimba au mwanamke kutoshika mimba kutokana na mirija ya uzazi kubanwa au msukumo unaosababishwa na ‘fibroids’, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus).

Mwanamke anapokuwa mjamzito na pia akawa na ‘fibroids’, wakati huo mwili huweza kusitisha kupeleka damu kwenye ‘fibroids’ na kuifanya isinyae. Kama hili likitokea, husababisha maumivu makali ya tumbo na kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa na baadaye mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.

Wakati wa kujifungua, kama ‘fibroid’ itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka au ikishindikana, mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliye tumboni.

Utawezaje kugundua kama una ‘fibroids’? Kama hakuna dalili yawezekana tu kwa kufanya vipimo. Dalili zikiwapo na kuhisi unalo tatizo la ‘fibroids’, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo kujua kama una ‘fibroids’ au la.
Daktari atafanya vipimo vya ‘Ultrasound’ (mionzi), ‘Hysteroscopy’ (kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke) na ‘Laparosopy’ (upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke).

Njia iliyozoeleka ya kuishi na ‘fibroids’ zinazotoa damu nyingi ni kuzilinda na si kuzitibu (monitor rather than treat them). Utashauriwa kupata uangalizi/uchunguzi wa mara kwa mara ingawa bado utahitaji kupata msaada zaidi kwa jinsi unavyojisikia.

Kuna njia kuu mbili za kutibu ‘fibroids’. Kutumia dawa (drug treatment). Mkusanyiko wa dawa zijulikanzo kama ‘GnRH analogues’ hupunguza kiwango cha ‘oestrogen’ mwilini na hivyo kusababisha ‘fibroid’ kusinyaa. Uchunguzi waonesha kuwa dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa ‘fibroid’ kwa aslimia 50. Pia dawa hizi hupunguza mzunguko wa hedhi.

Yashauriwa kwamba matumizi ya dawa za ‘GnRH analogues’ yasizidi miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa baadaye. Pia mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi, wiki chache baadaye ‘fibroids’ huanza kukua tena na mwanamke huanza kupata hedhi kama awali lakini ikiambatana na maumivu makali. Baadhi ya wanawake huwa hawapati hedhi tena kwa maisha yao yote.

Upasuaji unahusisha mambo yafuatayo: Kuiondoa ‘fibroid’ yenyewe na kuacha kizazi (myomectomy); kukiondoa kizazi kabisa (hysterectomy), kuzuia damu kwenda kwenye ‘fibroids’ (uterine artery embolisation). Pia iko njia isiyozoeleka sana ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni zikielekea zilipo ‘fibroids’ kwa ajili ya kuziua kwa kemikali maalumu.

Makala haya yameandaliwa kwa msaada wa jarida la Forever Living Products.
marobarnabas@yahoo.com

Ijumaa, 18 Aprili 2014

SABABU YA MAALIM GURUMO KUPOTEZA JICHO LAKE MOJA HII HAPA
























WAKATI Saluti5 ilipofanya ziara ya kwenda Masaki kijijini kwa mwimbaji Muhidin Maalim Gurumo aliyefriki Jumapili, ilipata mambo mengi mahsusi kutoka mwa gwiji huyo.

Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau  au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.
Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.
Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.
“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.
“Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.
“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akisimulia namna alivyopoteza jicho lake.

CHANZO: Saluti5.com






BREAKING NEWS: MELI YAZAMA ZIWA VICTORIA HIVI PUNDE





















Ni mwaka mmoja tangu Bi Kidude afariki dunia