promotion

Jumanne, 13 Mei 2014

MASTAA WA BONGO SASA KUMSHITAKI MPOKI, KISA KAWADHALILISHA



















































Komediani aliyebahatika kuwa maarufu Bongo, Mujuni Silvery 'Mpoki' yuko njiani kupandishwa kizimbani kufuatia mastaa waliodai aliwadhalilisha usiku wa Tuzo za Kili kucharuka na kwenda kwa 
mwanasheria wao, Ijumaa Wikienda lina ishu nzima. 


Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa wanaodaiwa kutinga kwa mwanasheria na kuandikisha maelezo ni hawa wafuatao: Mkurugenzi wa Aset Club inayomiliki Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka, mtangazaji wa runinga, Maimartha Jesse, Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.










































Aisha Mashauzi.

 Wengine ni Mbongo Fleva na mtangazaji, Vanessa Mdee, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’, Maria Sarungi na DJ Bonny Love.

 WADAI KUDHALILISHWA BILA KUPEWA NAFASI
Chanzo kilisema kwamba siku ya Tuzo za Kili, Mpoki akiwa MC wa shughuli hiyo, aliwadhalilisha kwa kutangaza ndani ya hadhara iliyohudhuria kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, mambo ambayo wenyewe hawakupata nafasi ya kujitetea (balansi).


































Asha Baraka.

 “Kule kwa mwanasheria wao, wote walidai kuwa, siku ile Mlimani City, Mpoki alikuwa akitangaza mambo yao, mengine ya siri, mengine si ya kweli, mengine ya udhalilishaji bila wao kupewa nafasi ya kujitetea kama mnavyofanya magazetini.

 “Wenyewe wanajua Mpoki hakutumwa na Kili kusema maneno yale bali aliamua yeye kama yeye tu. Ndiyo maana wameamua kushughulika na Mpoki na si mwingine,” kilisema chanzo hicho.


















































Maimartha wa Jesse.


 MADAI YAO YA MSINGI

Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba madai ya msingi ya mastaa hao  kisheria ni kudhalilishwa, kuzushiwa na kuchafuliwa mbele za watu, jambo ambalo liliwapa usumbufu mbele za jamaa zao, wakiwemo watoto na ndugu wengine waliokuwa wakifuatilia sherehe za utoaji wa tuzo hizo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki.


 KASHFA ZENYEWE KWA UFUPI

Soma kwa ufupi sana yale ambayo baath ya mastar hao waliambiwa siku ile  kwa ufupi sana lakini yenye kueleweka

.
 MAI; aliambiwa amezipiga jeki nido ilhali ana mtoto.
ASHA; aliambiwa kwa usiku huo alipendeza sana (make up) lakini akionekana kesho yake anaweza kupewa shikamoo kwa mabadiliko ya mwonekano.

 RAY; aliambiwa siku hizi amebadilika rangi, si kama zamani. Pia Mpoki alimwambia amesikia ameachana na Johari na yuko na Chuchu Hans.


































Ray Kigosi.

 Kwa upande wake, Isha Mashauzi alisema kuwa labda wenzake wameamua kumshtaki Mpoki lakini hawakuwa wamemjulisha. Mastaa wengine ambao simu zao ziliita bila kupokelewa ni Asha Baraka, Vanessa, Wema na DJ Bonny Love.

 

SOMA ALICHOSEMA MPOKI BAADA YA KUPIGIWA SIMU

Mpoki alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu malalamiko ya mastaa hao, katika hali ya kushangaza alisema hakumbuki nini kilitokea siku hiyo.

 “Kusema ule ukweli mimi sikumbuki chochote kile kilichotokea siku ile, we  nitajie majina ya hao watu niwapigie halafu baadaye ndiyo tutaongea,” alisema Mpoki akiweka sharti hilo wakati yeye ndiye aliyekuwa akiwananga jukwaani.

Hakuna maoni: