Amanda Rodgers Akiwa na Mumewe Sheba
Jumapili, 16 Machi 2014
Jumamosi, 15 Machi 2014
Ijumaa, 14 Machi 2014
Alhamisi, 13 Machi 2014
NDEGE WA AJABU WAIKUMBA BUKOBA, KINYESI CHAO CHAUA KUKU 516, NA MBUZI 12...!!!!!
Ndege wa ajabu wakiwa juu ya miti katika Kisiwa cha Musira kilichopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Ndege hao wamezua hofu kwa wakazi kutokana na kinyesii chao kudhuru mifugo na ndege.
Jumatano, 12 Machi 2014
Jumatatu, 10 Machi 2014
Jumapili, 9 Machi 2014
Jumamosi, 8 Machi 2014
Ijumaa, 7 Machi 2014
ADHA YA MVUA KUBWA JIJINI DAR ES SALAAM
Dereva wa Bodaboda, akiwa na abiria wake, wakinyanyua miguu kukwepa kulowa na maji ya mvua yaliyofurika kwenye barabara ya Mbozi, Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana. Mvua ya siku mbili tu tayari imeanza kuletakasheshe, si kwa wenye magari pia wenye bodaboda, watembea kwa miguu.
BIBI MJASIRIAMALI WA MAKOPO AENDESHA MAISHA DAR
Makopo yakiwa eneo la nyumba ya bibi huyo ambaye anaonekana kwa mbali akiondoka baada ya kuongea na paparazi wetu.
MZUNGU TAPELI ANASWA NA MAHELA KIBAO YA BANDIA HAPA BONGO
Kamanda Suleiman Kova
JAN ELOFF AKITOLEWA NJE YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM
JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY
Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.
Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyefahamika kwa jina la JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar.
Taarifa zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU, pamoja na Kutoa Euro Feki.
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukamatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.Kufuatia kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi 'kupigwa' na mzungu huyo basi wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.
Alhamisi, 6 Machi 2014
Jumatano, 5 Machi 2014
RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.
Akizungumza katika kikao maalum na Maafisa Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.
Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda.
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.
Katika ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.
MTOTO AUNGUZWA MIKONO YOTE MIWILI KWA KUDOKOA NJEGERE JIKONI P
Jumanne, 4 Machi 2014
JAMAA MWENYE UMRI WA MIAKA 47, AFUKUA KABURI KISHA KUTAKA KUFANYA MAPENZI NA MAITI YA BINTI ALIYEKUWA NA MIAKA 17
Jamaa kutoka Cambodia amefanya kitendo cha ajabu baada ya kufukua kaburi la binti wa Miaka 17 aliyefariki na kujaribu kufanya nae mapenzi(Huu ni mfano wa kaburi lililo fukuliwa)
Ni habari ya kusisimua ambapo jamaa alikuwa ameamua kufuakua kaburi la msichana mwenye miaka 17, kwa nia ya kufanya nae mapenzi, alishikiliwa na Polisi Baada ya kukutwa amelala juu ya Jeneza hilo huko Cambodia imethibitishwa
Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 47 aliyefahamika kwa jina la Chin Chean alikamatwa na wanakijiji baada kupatikana amefukua kabuli la binti, huku mwili huo wa marehemu ukiwa umeachwa wazi ndani ya jeneza hilo.
Chin Chien alilileleza Jeshi la Polisi kuwa alianza kuchimba kaburi hilo majira ya saa nne usiku , ikiwa ni siku moja baada ya kufanyika mazishi hayo ya binti huyo aliyekuwa na umri wa miaka 17
Jamaa huyo aliendelea kuchimba kaburi hilo hadi kufikia jeneza hilo na kufanikiwa kulifungua
Baada ya kumaliza kufukua na kufungua jeneza hilo jamaa huyo aliiambia polisi kwamba alifungua jeneza hilo na kutaka kufanya mapenzi na marehemu huyo akiwa katika Jeneza, lakini kutokana na udogo na ufinyu wa nafasi wa Jeneza hilo ilishindikana kwa yeye kufanya kitendo hicho.
Na baada ya kushindwa kufanya aliamua alale juu ya Jeneza huku likiwa wazi.
Wakizungumza wanakijiji walidai kwamba waliona Miguu ya Bwana Chean katika kaburi hilo mida ya saa kumi na mbili asubuhi na kuamua kuipa taarifa familia yake , walisema polisi
"Tunashindwa kuelewa kabisa kama huyu jamaa hapa kijijini alikuwa akimfahamu huyu Marehemu hata kabla hajafariki na kisha kuamua kufanya kitendo hiki" aliogea bwana Vutha
Lakini aliongeza kwa kusema kwamba Anamfahamu Bwana Chin Chean kuwa ni Mbwia unga na hufanya matendo ya ajabu ajabu, ambapo kuna siku alishawahi kutembea maeneo ya Pagoda akiwa mtupu bila nguo.
Jumatatu, 3 Machi 2014
WANANCHI WAMPIGA HADI KUMUUA KINYAMA MTUHUMIWA WA WIZI WILAYANI MAKETE
Mtuhumiwa wa wizi baada ya kupewa kichapo na wananchi, hapa ni kabla hajauawa.
Wananchi wenye hasira katika kata ya Tandala wilayani Makete mkoa wa Njombe wameamua kujichukulia sheria mkononi, kwa kumpiga hadi kumuua kinyama mtuhumiwa wa wizi ambaye walimkamata kwa madai kuwa ni mwizi wa mifugo
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao walikataa kutaja majina yao wala kupigwa picha, wamesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji cha Idege, ambapo kwa madai yao walimkamata na vithibitisho ambavyo ni kamba za kufungia mifugo (ng'ombe na mbuzi)
Wamesema wamechoshwa na vitendo vya wizi katika kata yao na wilaya kwa ujumla na kusema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na madai ya kuiba mifugo ya watu ambayo ni ng'ombe na mbuzi, katika maeneo ya Tandala, Ibaga, na huko Idege ambapo ndipo alipokuwa akiishi, hivyo vitendo hivyo vimewachosha
Mwandishi alipouliza kama wanauhakika kuwa mtuhumiwa huyo ndiye mwizi wa mifugo walisema ndiyo, lakini hawakutaka kuithibitisha tuhuma hiyo, na kusema ili iwe fundisho kwa wengine watawaua watuhumiwa wote wa wizi watakaowakamata!
"Dawa itakuwa hii, tumechoka kuibiwa, kila mwizi tutakayemkamata dawa itakuwa hii" walisema wananchi hao kwa jazba
Mtandao huu ulishuhudia wananchi hao wakimpa kipigo cha mbwa mwizi mtuhumiwa huyo kwa mateke, fimbo, na mawe jambo lililompelekea mtuhumiwa huyo kufariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi
Mtuhumiwa huyo wakati akiendelea kupigwa kulikuwepo na kamba anazotuhumiwa kuwa ni za kufungia mifugo anayoiiba, nguo, begi na mablanketi pamoja na unga
Baada ya taarifa za mauaji hayo kufikishwa kituo cha polisi Makete, polisi walifika eneo hilo na kuuchukua mwili wa marehemu ambao ulionekana kujeruhiwa zaidi sehemu ya kichwa, na kusema taarifa zaidi zitatolewa

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)