promotion

Jumamosi, 25 Aprili 2015

Tetemeko la ardhi lawaua watu 560 Nepal

mcharoman blogy fahar yako mtanzania


Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo lililo magharibi mwa Nepal karibu na mji mkuu wa Kathmandu .Maafisa wa polisi wanasema kuwa zaidi ya watu 560 wamethibitshwa kufariki huku wengi wakiwa hawajulikani waliko na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka..
Shirika la utafiti la Marekani liliseme kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.9 lilikumba eneo lililo umbali wa kilomita nane mashariki mwa Pokhara magharibi mwa mji mkuu wa Kathmandu.
Kuna ripoti za uharibifu wa majengo. Idadi ya watu waliokufa au kujeruhiwa haijulikani.
Tetemeko la ardhi mjni Nepal lenye vipimo vya richa 9.7
Picha za majengo yaliyokuwa yameporomoka pamoja na mahekalu ya miaka mingi iliyopita zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii.
Mawasiliano ya simu nayo yameharibiwa.
Walioshuhudia walisema kuwa watu walikimbia nje ya majengo muda mfupi baada ya tetemeko hilo kutokea.
Tetemeko la ardhi Nepal
Mitetemeko mingine midogo imesikika kaskazini mwa India pamoja na nchini Pakistan.
SOURCE BBC SWAHILI

Hakuna maoni: