promotion

Jumamosi, 25 Aprili 2015

UCHAGUZI WA RAIS NCHINI TOGO UNAFANYIKA LEO JUMAMOSI

mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Rais wa Togo wa sasa anayewania kurudi madarakani, Faure Gnassingbe alipokuwa akipiga kura yake mapema hii leo.


Raia wa Togo wakiwa katika vituo vyao vya kupigia kura.
Uchaguzi wa Rais wa Togo unafanyika leo Jumamosi. Wananchi wa Togo wamefika mapema kwenye vituo vyao vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais Mpya wa nchi hiyo.
Tume huru ya uchaguzi ya Togo imetangaza kuwa, raia wapatao 3,590,258 ndio wanatarajiwa kupiga kura hiyo kwa mujibu wa katiba ya Togo.
Aidha vituo vya kupigia kura 8,994 vimeanza kufunguliwa saa moja asubuhi kwa wakati wa Togo ili kuwaruhusu wananchi kuanza kupiga kura na kwamba zoezi hilo litaendelea hadi saa kumi alasiri leo.
Wananchi wa Togo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura hii leo katika uchaguzi wa Rais ambao huwenda ukambakisha uongozini kwa kipindi kingine cha tatu cha miaka mitano Rais wa hivi sasa wa nchi hiyo, na hivyo kuiweka familia yake madarakani kwa karibu miaka 50.
Rais Faure Gnassingbe wa Togo aliingia madarakani mwaka 2005, baada ya baba yake ambaye aliiongoza Togo kwa miaka 38 kuaga dunia kwa ugonjwa wa moyo. Faure Gnassingbe anachuana vikali katika uchaguzi wa Rais wa leo huko Togo na mgombea wa upinzani Jean Pierre Fabre kutoka Muungano wa Taifa kwa ajili ya Mabadiliko

Hakuna maoni: