mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za
kifo cha mtumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) na Chama cha TANU na Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa
Afrika kwa miaka mingi, Brigedia Hashim Mbita.
Mzee
Mbita ambaye amekuwa anauguza afya yake kwa muda sasa amefariki asubuhi ya leo,
Jumapili, Aprili 26, 2015 mjini Dar Es Salaam.
Kufuatia
taarifa za msiba huo, Rais Kikwete ameelekeza Serikali na Jeshi kushirikiana na
familia kusimamia msiba huo na kuandaa mazishi ya Mzee huyo.
(N.B.
Salamu Kamili za Rambirambi za Mhe. Rais zinafuatia baada ya muda)
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni