mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Wanasiasa
hapa nchini wametakiwa kufanya mikutano yao kwa amani na utulivu ili kuepusha
vurugu na migogoro inayoweza kujitokeza kwa wananchi pindi wanapofanya mikutano
yao kwa jamii.
Kauli hiyo
imetolewa mapema hii leo na kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa simiyu (ACP) gemini
mushi wakati akitoa ufafanuzi wa mikutano ya kisiasa inayoendelea mkoani humo.
Hata hivyo
kamanda mushi amesema kuwa ni vema wanasiasa wote wakafanya kazi shughuli zao
kwa ustaarabu ili kujiepusha na uvunjifu wa amani kwenye maeneo yote
watakayopita kwa lengo la kuzungumza na wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni