mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Wakati hatma ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ikiwa haijajulikana, mbunge huyo jana alihudhuria mkutano wa Bunge la 19, huku alitulizwa na kwa Spika wa Bunge, Anna Makinda, asimbane naibu waziri.
Spika wa Bunge, Anna Makinda. |
Wakati hatma ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ikiwa haijajulikana, mbunge huyo jana alihudhuria mkutano wa Bunge la 19, huku alitulizwa na kwa Spika wa Bunge, Anna Makinda, asimbane naibu waziri.
Zitto alitulizwa baada ya kumtaka Spika Makinda amwamuru Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwange, afute kauli yake aliyodai
kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleima Bungara, hajui hesabu.
“Mheshimiwa Spika tunataka waziri afute kauli ya kwamba, mbunge
hajui hesabu sababu tunaiuliza serikali maswali itujibu vizuri,” alisema
Zitto.
Hata hivyo, Spika Makinda alimwambia Zitto kuwa siyo kazi yake kwa kuwa yeye (Zitto) siyo Spika.
“Zitto hiyo siyo kazi yako,” alijibu Spika kwa kifupi.
Hatua ya Bungara kuelezwa kwamba, hajui mahesabu ilifuatia baada ya
kuuliza swali la nyongeza kuhusu masuala ya mrahaba kutokana na gesi ya
Songosongo.
Awali Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Charles Kitwanga,
alisema Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ina tozo zake inazotoza kwa
mujibu wa sheria.
Dk. Kitwanga alisema moja ya tozo hizo ni ushuru wa huduma wa
asilimia 0.3 ya mapato yote, ambayo hulipwa kila robo mwaka na kampuni
ya Pan Africa Energy, ambayo ndio inayouza gesi ya Songosongo.
Alisema kwa kipindi cha mwaka 2012 hadi Desemba,mwaka jana, halmashauri hiyo imelipwa Sh. bilioni 1.37 kutoka kampuni hiyo.