promotion

Alhamisi, 19 Machi 2015

PICHA MBALIMBALI ZA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI INAYOENDELEA MKOANI MWANZA INAYORATIBIWA NA TASAF KWA KANDA YA ZIWA

mcharoman blogy fahar yako mtanzania

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka katika mkoa wa simiyu, wakiwa katika semina ya siku 4 inayoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ambpo semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa uelewa juu ya mpango wa Tasaf awamu ya tatu yenye lengo la kunusuru kaya maskini.


Washiriki wakifuatilia mada kutoka kwa waendesha semina, maafisa kutoka Tasafa makao makuu, Semina hiyo ilikuwa ikifanyikia Jijini mwanza katika ukumbi wa Nyakahoja. semina hiyo ambayo ni semina ya kazi ilikuwa ikijumuisha waratibu wa tasaf kutoka wilayani, maafisa ushauri na usimamizi ikiwa pamoja na wahasibu tasaf wilayani.


Maofisa wa TASAF ngazi za wilaya, kutoka katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, pamoja na Mara.



Mkurunge Mtendaji wa TASAF nchini Ladislaus Mwamanga akiongea na washiriki wa semina, wakati akifungua semina hiyo ambayo imewahusisha waandishi wa habari kanda ya ziwa kutoka katika mikoa ya Mara, Simiyu, pamoja na Mwanza.