mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Umahiri wa hali ya juu wa uimbaji ulioneshwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye na msanii wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’ juzikati walikuwa kivutio kwa waombolezaji waliokuwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar ambako mwili wa marehemu Kapteni John Komba ulikuwa ukiagwa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye (katikati) akiimba wimbo maalum na wasanii wa muziki wa dansi
Mbali na wasanii kibao waliopanda jukwaani kwa nyakati tofauti kuimba nyimbo mbalimbali alizotunga marehemu kipindi cha msiba wa Mwalimu Nyerere huku wakichomekea jina lake pale linapotajwa jina Nyerere, Nape na Nisha ni kati ya mastaa wasiofanya muziki lakini walionesha kuwa wana vipaji.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa viwanja vya Karimajee.
Baadhi ya watu waliokuwa uwanjani hapo walionekana kutoamini kama waliokuwa wanaimba ni wale wanaowafahamu na kutokana na hisia walizokuwa nazo, wengi walijikuta wakibubujikwa na machozi akiwemo Rais Jakaya Kikwete.
Hata hivyo, Nape anafahamika kuwa ni mwanamuziki aliyeikacha fani hiyo na kujiingiza kwenye siasa na Nisha aliwahi kujaribu kufanya muziki lakini dizaini kama aliona haulipi hivyo akahamia kwenye filamu.