promotion

Jumatano, 4 Machi 2015

NI VILIO NA SIMANZI KWA MAENEO YA KAHAMA NA TANZANIA KWA UJUMLA KKUTOKANA NA WATU 38 KUFARIKI DUNIA KUFUATIA MVUA KALI ILIYONYESHA WILAYANI KAHAMA USIKU WA KUAMKIA LEO

mcharoman blogy fahar yako mtanzania




miti ikiwa imeny'oka baada ya mvua hiyo

mkuu wa wilaya ya kahama na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo akiongea na wananchi na eneo hilo

mchungaji akitoa sala fupi kwa tayari kuwahifadhi ndugu zetu waliopoteza maisha

Watu 38 wamefariki dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mwakata Kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.


Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao.

Kamanda Kamugisha amesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwani kutokana na majeruhi wengine kuwa na hali mbaya na kwamba majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika.

Amesema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa shinyanga inakaa jioni hii ili kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa wahanga hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.

Akiwa eneo la tukio Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza kufanywa na viongozi wa eneo hilo.

Kahama FM imefika katika eneo la tukioa na kushudia nyumba za kaya mbalimbali katika kijiji hicho zikiwa zimebomoka na nyingine kuezuliwa mapaa huku hali ya mazao na miti ikiharibiwa vibaya na mvua hiyo ambayo pia imeuwa mifugo.
Wakati huohuo mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesyaamewaomba Watanzania wote wenye Mapenzi mema kutoa misaada ya kibinadamu kwa familia zilizokumbwa na maafa ya mvua ya mawe iliyopoteza maisha ya watu 38 huku wengine wakijeruhiwa katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama.

Mpesya amesema katika kijiji hicho mazao yote ya chakula na biashara hadi miti imeng’olewa huku ikiangusha nyumba hali iliyosababisha hata mazao yaliyokuwa yamehifadhiwa ndani kuaharibika.
Amefafanunu kwamba hata shughuli za mazishi ya miili 38 ya watu waliopoteza maisha ambapo kwenye baadhi ya familia wamefariki wote, yamekuwa magumu kwani watu wanaozika hawana chakula.
Mpesya amewaomba watu binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na yale ya dini pamoja na makampuni kutoa msaada wa haraka kwa kuchangia kitu chochote kupitia ofisi yake au radio kahama fm kwa ajili ya kuwanusuru wahanga hao.
Wanawakekwanza.blogspot inaungana na wafiwa wote katika kuomboleza msiba huo mkubwa na inawaomba watanzania wenye mapenzi mema kumuunga mkono Mpesya katika kutoa misaada ya kibinadamu.