mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama ishara ya uzinduzi huo, tayari kwa matumizi. |
Rais Kikwete akitoa hotuba fupi kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Azam Ltd, Said Bakressa akipanda ngazi kwa ajili ya kuongea machache kwa waalikwa na mgeni rasmi, Rais Kikwete.
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Tido Muhando akiongea jambo kwenye uzinduzi huo.
Rais Kikwete akishuka ngazi baada ya kumaliza kuangalia moja ya studio iliyopo kwenye moja ya magari ya kurushia matangazo.
Waziri wa Habari,Vijana ,Michezo na Utamaduni, Dk Fenela Mukangara akitelemka kwenye ngazi mara baada ya kumaliza kuangalia moja ya mitambo ya kuendeshea TV hiyo.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Cuf kwenye uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kushoto), akiteta jambo na Shekhe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Mwenyekiti wa Chama cha Cuf, Prof. Ibrahim Lipumba akimtunza mmoja wa wafanyakazi wa Azam akiyekuwa akiigiza baadhi ya sauti za viongozi kwenye hafla ya uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Fedha Nchemba, akisalimiana na wasanii wa vichekesho, Mpoki na Joti.
Baadhi ya mafundi mitambo wa Azam wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya chumba cha kurushia matangazo.
Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Barnaba na Mwasiti wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini shughuli za uzinduzi huo.

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete, mapema jana amefanikisha uzinduzi wa Kituo cha Runinga cha Azam kilichopo maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Rais Kikwete, alisema amefurahishwa sana na ubora wa studio hizo kwani uwepo wake umeweza kututoa kimasomaso Watanzania wote kwa ujumla kwani studio hizo zina hadhi namba moja kwa Afrika Mashariki na Kati.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)