JUMLA ya watoto kumi na nane wamezaliwa usiku wa mkesha wa sikukuu ya Christmas katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani shinyanga ambapo kati ya hao 10 niwakiume na wakike 8.
Akizungumza
na Kijukuu Blog leo mganga mfawidhi hospital ya wilaya ya Kahama Dkr,Charles
Rwaikeza,alisema kuwa jumla ya watoto kumi na nane wamezaliwa usiku wa mkesha
wa sikuku ya Christmas wote wakiwa wamezaliwa salaama bila matatizo yoyote.
Alisema
kuwa alipokea takwimu za watoto waliozaliwa kutoka kwa wakunga waliokuwa zamu
ambapo ilikuwa jumla ya watoto kumi nane wamezaliwa wakiwa na afya njema ambapo
watoto wakike 8 pamoja na watoto wakiume walikuwa ni 10.
Hata
hivyo Rwaikeza amewataka wakinamama waepuke kujifungulia nyumbani badala yake
pindi wanapojihisi mabadiliko ya kimwili wakati wa ujauzito wawahi katika
hospital ama zahati zilizo karibu nao ili kupata matibu ikiwa ni njia mojawapo
ya kujifungua salaama.
Aliongeza
kuwa pindi wakimama wajawazito wanapokuwa hospitalini wakisubili wakati wa
kujifungua na kupata usumbufu kutoka kwa wauguzi wasisite kufika katika ofsi ya
mganga mfawidhi kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yayokuwa
yamejitokeza kwa wauguzi wa zamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni