Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Magreth Nakainga amemvua
madaraka Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyakabale, Josephat Msafiri kwa
kukiuka miiko ya kazi yake na kulewa wakati wa kazi.
Mkurugenzi
huyo aliamua kuchukua uamuzi huo jana kutokana na tukio lililotokea
Juzi la daktari huyo kufunga kituo cha afya na kuacha wagonjwa wakiwa
wamezidiwa, kisha kwenda kunywa pombe jambo lililowalazima kumchapa
viboko akiwa baa.
“Tumeshamchukulia
hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka yake ili iwe
fundisho kwa watumishi wengine wa Serikali,” alisema Nakainga.
Alisema kitendo alichokifanya kimeidhalilisha taaluma ya afya na madaktari kwa ujumla.
Alisema tabia kama hizo hazitavumilika kwa mtumishi yeyote atakayekiuka maadili ya kazi.
Pia
alisema amepeleka wahudumu wa afya wakiwamo wauguzi wawili na daktari
mmoja katika zahanati hiyo na huduma zinaendelea vizuri.
Alipopigiwa
simu jana ili azungumzie uamuzi huo, daktari huyo alianza kumlaumu
mwandishi aliyeandika habari ya tukio hilo akisema kuwa amemharibia
kazi.
“Sikutegemea
kama wewe uko hivyo, sasa nimekujua kumbe uko hivyo, Mungu mkubwa,
yaani mmepigiwa simu na watu na kuamua kuja kuniharibia,” alisema Dk
Msafiri na kukata simu kisha akaandika ujumbe uliosema:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni