promotion

Ijumaa, 14 Novemba 2014

‘Silaha, dawa za kulevya zinaingiaje?’





MBUNGE wa Viti Maalum Moza Abeid (CUF) ameihoji serikali na kutaka itoe maelezo ni kwa njia gani zinatumika kuingiza bidhaa mbalimbali nchini kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na uingizaji wa dawa za kulevya.
Akiuliza swali la nyongeza Moza alitaka kujua ni silaha zinazozagaa nchini zinatoka wapi na nani wanaoziingiza
Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itaruhusu ukaguzi wa magari ya mizigo yanayokwenda nje ili kuelewa mizigo iliyomo ni ya aina gani.
“Kuna magari ya mizigo yanayopita kwenye vituo bila askari kuyakagua na yanakuwa yamefungwa lakiri(seal) ..
“Je ni lini serikali itaruhusu ukaguzi wa magari hayo ili kuelewa mizigo iliyomo ni ya aina gani” alihoji Moza.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu,Taawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Elimu (TAMISEMI) Kasim Majaliwa alisema kuwa magari yote yanayopita nchini kwenda nchi nyingine yanafungwa lakiri (Seal) hivyo si rahisi kuwa na mzingo unaoweza kushushwa njiani.
Majaliwa alisema ukaguzi wa mizigo unaofanywa na askari unaongeza gharama za kufanya biashara kwakuwa huchukua muda mrefu na hivyo mizigo kushindwa kufikishwa kwa wateja kwa wakati.
“Ucheleweshwaji wa mizigo unatokana na ukaguzi usiokuwa wa lazima, unaifanya bandari yetu kuwa na gharama kubwa ya kupitisha na kusafirisha mizigo ukilinganisha na bandari nyingine za nchi jirani” alisema Majaliwa.

Hakuna maoni: