promotion

Alhamisi, 23 Oktoba 2014

WASANII 7 MATAJIRI AFRIKA




































Baada ya wiki iliyopita kuwaletea marais ambao watoto wao nao wameshika nafasi hiyo katika nchi zao, leo nakuletea wasanii saba matajiri Afrika.
Youssou N’dour:
Mkongwe toka Senegal, aliyezaliwa mwaka 1959, ndiye tajiri kwa wanamuziki wa Afrika, akimiliki chombo cha habari kikubwa nchini mwake, ni mwimbaji, mtunzi mwigizaji, mfanyabiashara na mwanasiasa, aliwahi pia kuwa Waziri wa Utamaduni na Maliasili nchini Senegal.
P.Square:
Peter na Paul Okoye toka Nigeria, wanashika nafasi ya pili kwa utajiri, barani Afrika kwa zaidi ya dola 150,000/= kwa shoo. Kwa sasa wanafanya kazi na lebo ya  Akon ‘’Konvict muziki’’ na pia walishafanya kazi na Kampuni ya Universal Music South Africa.
Dapo Daniel Oyebanjo
‘’D’banj’’ alizaliwa nchini Nigeria mwaka 1980, ni mwanamuziki na mjasiriamali, ameshawahi kuchukua tuzo kadhaa zikiwemo za MTV, BET na nyinginezo.
Antoine Christophe Mumba “Koffi Olomide’’
Mzaliwa wa Jamhuri ya Watu wa Kongo, alizaliwa mwaka 1956, ni mmoja wa wanamuziki wa zamani ambao hawajawahi kuchuja tangu aanze muziki.
Salif Keita:
Alizaliwa mwaka 1949, ni mmoja wa wasanii matajiri Afrika mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) ana sauti nzuri na anamiliki bendi yake, kisiwa na kiwanja kikubwa nchini Ufaransa.
Fally Ipupa Nsimba:
Mwanamuziki toka Jamhuri ya Watu wa Kongo, alizaliwa mwaka 1977, aliwahi kuwa katika bendi ya Koffi Olomide, ni mwimbaji, mtunzi, mpiga gitaa, anayesifika kwa kukata mauno awapo jukwaani, amewahi kushinda tuzo kadhaa za MTV, Kora na nyinginezo.
Innocent Ujah Idibia
‘’2face Idibia’’ alizaliwa  Jimbo la Jos nchini Nigeria, ni mtunzi, mwimbaji na mtayarishaji wa muziki, amewahi kushinda tuzo kadhaa zikiwemo za MTV, Channel O, BET, Kora na MOBO.

Hakuna maoni: