Mapigano yalianzia sehemu hii ya kumbukumbu ya vita tukio linalodhaniwa kuwa la kigaidi nchini Canada.
Mwanajeshi ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nje na ndani ya Bunge la Canada mjini Ottawa katika tukio linalodhaniwa kuwa la kigaidi, ambapo mji huo mkuu upo chini ya ulinzi mkali wa Polisi na wanajeshi.
Kufuatia tukio hilo waziri mkuu wa nchi hiyo Stephen Harper amehutubia Taifa hilo na kutaka wananchi watulie huku akisisitiza kuwa Canada haitowaachia magaidi watambe.
Shambulio limekuja saa kadhaa baada ya Canada kukemea vikali vitendo vya kigaidi.siku ya jumatatu.
Vyombo vya usalama nchini humo vimethibitisha kuwa mshambuliaji mmoja ameuawa na ametambuliwa kwa jina la Michael Zehaf-Bibeau. Kufuatia tukio hilo waziri mkuu wa nchi hiyo Stephen Harper amehutubia Taifa hilo na kutaka wananchi watulie huku akisisitiza kuwa Canada haitowaachia magaidi watambe.
Shambulio limekuja saa kadhaa baada ya Canada kukemea vikali vitendo vya kigaidi.siku ya jumatatu mwanajeshi mwingine aliuawa katika shambulio la kushtukiza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni