Jumanne, 22 Julai 2014
Linah aeleza maana ya 'Ole Themba', alichomaanisha na jinsi atakavyofanya kazi na kampuni mpya ya kimataifa
‘Ole Themba’ ni jina la wimbo wa Linah ambao hivi sasa umepata nafasi sana kwenye vyombo vya habari na umekubalika na wengi kwa ubora wa audio na video. Lakini maana na alichokimaanisha moja kwa moja ni kitendawili kwa wengi.
Msanii huyu wa kike ameelezea maana ya wimbo ambao umepewa jina la lugha ya Kizulu ‘Ole Themba’.
“Hiyo Ole Themba ni Kizulu, na maana yake ni tumaini. Kwa hiyo Ole Thembana maana yake ‘tumaini langu’ hicho ndicho nilikuwa nakimaanisha. Lakini all in all inahusu mapenzi, namwambia mpenzi wangu kuwa yeye ndiye tumaini langu na nini. Nampetipeti waswahili wanasema namjaza yaani” Amesema Linah.
Ameongeza kuwa melody na jina la wimbo huo alipewa na Uhuru wa Afrika Kusini, sehemu aliyorekodia.
Akizungumzia jinsi atakavyofanya kazi na kampuni yake mpya ya No Fake Zone akiwa kama msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kufanya kazi na kampuni hiyo, atakuwa anafanya kazi akiwa Tanzania na kwamba recording na mambo mengine yatamlazimu kwenda Afrika Kusini kuyakamilisha.
“Ile kuagwa nilikuwa naagwa hapa katika kikundi nachofanyia kazi lakini NFZ wapo kote, wanabranch yao hapa Tanzania na ndio maana imekuwa rahisi kufanya kazi na mimi. Na nimekuwa msanii wa kwanza kufanya kazi na kampuni hiyo kwa Afrika Mashariki. But it’s an International company.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni