promotion

Jumanne, 22 Julai 2014

Sakata la miili Tanzania,wanane mbaroni



































Mabaki ya miili iliyotupwa eneo la Bunju Dar es Salaam


Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.
Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.
Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.


































Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova

Watu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio l a kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la Dsm
Huku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.
























Moja ya viungo vilivyokutwa katika eneo hilo vikiwa ndani ya mifuko ya malboro

Hakuna maoni: