Majeraha ya maji ya moto aliyopata Bw. Adam Rashid.
Baada ya mwanaume huyo kumaliza kuoga na kutoka nje, inadaiwa mkewe mkubwa alijitokeza akiwa amebeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto, yanayodaiwa kuwa yalitakiwa kutumika kwa ajili ya kupikia wali na kumwagia tumboni na sehemu za siri, huku akiendelea kumtolea maneno ya kashfa.
MAJERUHI ALONGA NA UWAZI
Akiwa amelazwa katika wodi namba tatu kwenye hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam, majeruhi Adamu Rashid alisema Julai 16 mwaka huu alienda nyumbani kwake akiwa ameandamana na mke wake mdogo, lakini akashangazwa na kitendo cha bi mkubwa kuanza kubwata na kumwuliza alichokifuata, kana kwamba amesahau kama pale ni kwake na wote ni wake zake.

“Baada ya kunimwagia maji, mke wangu mdogo alilia sana kwa uchungu, majirani wakanichukua na kunipeleka Polisi ambako tulimkuta bi mkubwa akiwa anaandikisha maelezo kuwa mimi nimempiga, kuona vile askari walimgeuzia kibao na kumwingiza ndani kwa ajili ya mahojiano zaidi.”
Adam Rashid akifunguka kuhusu mkasa uliompata
MKE MDOGO NAE
“Ndugu mwandishi, mimi na mume wangu tulienda hadi kwa mke mkubwa bila wasiwasi maana na mimi pale ni kwangu kwa sababu nyumba ya mume wangu halali, lakini tulipofika tuliambulia maneno machafu na kejeli.

Mke mkubwa alihoji kwa jeuri kitu gani tulichokifuata pale, mume wangu alikuwa akimjibu kuwa hapa nipo kwangu na huyu niliyekuja naye ni mke wangu halali, mbona unanifanyia mambo ambayo siyaelewi, yule hakuelewa, aliendelea tu na maneno yake machafu.”
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Ilala, SACP Marieth Minagi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa huyo anashililiwa katika kituo cha polisi Wilaya ya kipolisi Ukonga na amefunguliwa jalada na kupewa namba RB/STK/9438/2014 KUJERUHI na uchunguzi unaendelea.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni