Mfanyakazi wa ndani ‘hausiboi’, Lawrence Flavian (22) aliyemuua mtoto wa bosi wake na kumla ubongo.
YALE mauaji ya kutisha ya mtoto Francis Fortunatus Urassa (9) aliyeuawa kwa kucharangwa mapanga kichwani hadi ubongo kutawanyika na kuliwa na mfanyakazi wa ndani ‘hausiboi’, Lawrence Flavian (22) ambaye naye alijikata uume pia akaula, akafa, bado yanatikisa nchi.
Marehemu mtoto Francis Fortunatus Urassa (9) enzi za uhai wake.
AKUTWA AMEJIKATA NYETI, AILA
Mashuhuda hao walisema walianza msako mkali na dakika chache baadaye walimkamata mtuhumiwa huyo akiwa amejikata nyeti na alikuwa akizitafuna kama nyama ya mshikaki.
Mashuhuda hao walisema walianza msako mkali na dakika chache baadaye walimkamata mtuhumiwa huyo akiwa amejikata nyeti na alikuwa akizitafuna kama nyama ya mshikaki.
JESHI LA POLISI LINAVYOSEMA
Akizungumza na Uwazi kuhusu mauaji hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Robert Boaz alisema mtuhumiwa huyo alishikwa na mapepo.
Alisema mtuhumiwa alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospital ya Kilema, Moshi akiwa hajaanza kupatiwa matibabu.

Mtoto Francis Fortunatus Urassa (9) aliyeuawa kwa kucharangwa mapanga.
Kwa mujibu wa baba huyo, mtoto wake alifikwa na mauti hayo muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kutoka shule ambako alisahau kitabu cha masomo. Marehemu alikuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Marangu Hills Academy.
Baba: “Baada ya kuingia ndani alimkuta muuaji akiwa chumbani, yeye akaenda kuchukuwa kitabu lakini ghafla muuaji alimfuata na kumfungia ndani na kuanza kumpiga.
“Kwa sababu mtoto wangu alipiga kelele, majirani walijitokeza, lakini muuaji aliwafukuza. Wakati huo tayari mwanangu alishaanza kulegea mwili kutokana na kipigo.
“Kwa sababu mtoto wangu alipiga kelele, majirani walijitokeza, lakini muuaji aliwafukuza. Wakati huo tayari mwanangu alishaanza kulegea mwili kutokana na kipigo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa akiwa hoi.
mfanyakazi wa ndani ‘hausiboi’, Lawrence Flavian (22)“Baada ya kuwatimua majirani, muuaji alimtoa mwanangu ndani na kwenda kutekeleza mauaji hayo kwa panga sasa katika shamba la mahindi ambalo lipo karibu na shule ikiwa ni umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwangu.”
SIKU MOJA KABLA YA MAUAJI
Kwa mujibu wa mzazi huyo, siku moja kabla ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alionekana kuchanganyikiwa akili kama ana mapepo lakini alifanyiwa maombi na kurejea katika hali ya kawaida hivyo kuondoa wasiwasi juu ya kile ambacho kilitokea.

MASHUHUDA SASA
Kwa mujibu wa mashuhuda ambao wanaamini mtuhumiwa alirukwa akili, wakati marehemu Francis anapigwa walifika nyumbani hapo lakini mtuhumiwa aliwakimbiza, wakakimbia wakijua ni kipigo cha kumrekebisha mtoto ingawa haikuwa kawaida ya mtuhumiwa huyo kufanya hivyo.

Walisema baadaye wakagundua kuwa mtuhumiwa alitoka nje na mtoto huyo hadi kwenye shamba la mahindi ambako alimcharanga mapanga bila huruma kiasi cha kuutawanya ubongo wa mtoto huyo aliyekuwa na ndoto za kuwa rubani wa ndege.
ALA UBONGO, AKIMBILIA KICHAKANI
Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa, mtuhumiwa aliifikia hatua ya kuula ubongo huo uliokuwa umesambaa chini kisha akakimbilia kwenye kichaka jirani na nyumba kujificha ili asikamatwe.
Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa, mtuhumiwa aliifikia hatua ya kuula ubongo huo uliokuwa umesambaa chini kisha akakimbilia kwenye kichaka jirani na nyumba kujificha ili asikamatwe.
Mmoja wa mashuhuda hao alisema, mtuhumiwa alimuua mtoto huyo wa bosi wake kwa kuanza kumpiga kwa panga kisha kumtoboa kichwani na ubongo ulipomwagika akauzoa kwa mikono na kunywa kama uji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni