Jumamosi, 1 Machi 2014
Ijumaa, 28 Februari 2014
MAISHAPLUS YATINGA KIJIJI CHA IGULA, MCHAKATO KUWAPATA WASHINDI TISA ... 2014
Washiriki 20 wa Maishaplus 2014 wakiwa katika Kijiji cha Igula kata ya Kihologota Tarafa ya Isimani
Washiriki wa Maishaplus wakiangalia kazi yao waliyoifanya ya Ujenzi wa Nyumba iliyobomoka ya Bw. Benad Mfwala katika kijiji cha Igula Kata ya Kihologota Tarafa ya Isimani Mkoani Iringa.
Washiriki wa Maishaplus wakiendelea na kazi za kijamii za ujenzi wa nyumba katika kijiji hicho cha Igula
Washiriki wa maishaplus wakiendelea na kazi ya kuchimba msingi wa choo cha shule ya msingi ya Igula iliyopo kata ya Kihologota Tarafa ya Isimani Mkoani Iringa.
Ni choo cha shule ya msingi ya Igula ambacho washiriki wa maishaplus hao wameweza kukiweka choo hicho taika hali ya usafi kutofautisha na hali ya mwanzo katika choo hicho
Maishaplus 2014 yatinga katika Kijiji cha Igula Kata ya Kihologota kilichopo Tarafa ya Isimani Mkoani Iringa katika mchakato wa kuwapata watu 9 kati ya washiriki 20 waliyoshiriki katika mchezo huo ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia shilingi milioni 25Tsh. Kauli mbiu ya Maishaplus ya mwaka 2014 Ni "REKEBISHA", kwa lengo la kuwataka vijana kubadilika kwa kurekebika katika maisha yao na kuwa na mawazo chanya yenye maendeleo.
Alhamisi, 27 Februari 2014
Jumatano, 26 Februari 2014
ABAMBWA AKIIBA KANISANI LAIVU BILA CHENGA, AGEUZWA BUCHA [MAPICHA]
Wanachuo wakikagua baadhi yavitu alivyokutwa navyo Emmanuel.Kijana anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea kipigo ‘hevi’ baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar.
Emmanuel baada ya kupokea kichapo cha nguvu kutoka kwa wanachuo.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo jamaa huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo ambao kabla ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.
“Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku watu wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu, wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo, sasa huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya kukamatwa kwa jamaa huyo.
Emmanuel akiwa mikononi mwa wanachuo wenye hasira.
Wanachuo hao, wakionekana kupania kumfundisha adabu na kumwachisha Emmanuel udokozi, walikuwa wakimhoji maswali huku wakimwangushia kipigo mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka damu nyingi iliyotapaa sakafuni kama buchani.

Emmanuel akiwa na vitu vya wizi alivyokutwa navyo
Kama kawaida, mapaparazi wetu hawakutaka kuishia kuangalia kipigo tu, waliwaita baadhi ya wanachuo walioibiwa mali zao na mashuhuda waliomuona jamaa huyo akiiba na kueleza mchezo mzima ulivyokuwa. “Nilikuja hapa chuoni saa tisa (alasiri) nikaelekea mapokezi na baadaye darasani.
Nilipofika hapo, nikamuona mtu akisimama ghafla, nikashtuka lakini sikutaka kuwa na wasiwasi sana, nilidhani ni mwanachuo wa hapa,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na kuendelea:
“Nikaondoka hapo na kupanda juu (ghorofani). Moyo wangu ukawa mzito, ghafla nikajikuta nikishuka ngazi na kurudi kule mapokezi. Nilipofika mapokezi, yule mtu niliyemuona pale hakuwepo, nilipoanza kumtafuta, nikaona akielekea getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo ndipo nilipoanza kupiga kelele za mwizi, naye akaanza kukimbia mpaka alipokamatwa,” alisema Adolphina.
Jamaa huyo alipopekuliwa begi alilokuwa nalo alikutwa na vyeti mbalimbali vya shule ya sekondari ya mkoani Mbeya, cheti cha kuzaliwa, cheti cha TRA na vyeti vingine vingi, vyote vikiwa si vyake. Mbali na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za mashine za ATM zikiwepo za CRDB, NMB na NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa anazitumia kwa ajili ya kuchukulia ‘mkwanja’ kutoka katika akaunti za watu.
Alipopekuliwa zaidi mifukoni mwake alikutwa na simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi 360,000 na Nokia Asha yenye thamani ya shilingi 150,000, ambazo zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku chache zilizopita.
Askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama – Mabatini ndiyo walimuokoa jamaa huyo mikononi mwa wanachuo hao ambapo walifika eneo la tukio baada ya kujulishwa na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa huyo akisulubiwa kwa hasira

Jumamosi, 22 Februari 2014
Ijumaa, 21 Februari 2014
MKULIMA AFARIKI DUNIA WAKATI AKISHINDANA NA WENZAKE KUNYWA POMBE
Alhamisi, 20 Februari 2014
MAMA WA MAKAMO AGARAGARA HADHARANI BAADA YA KUTAPELIWA T.SH MILIONI 5.4 MJINI MOSHI LEO
MATAPELI HAO WALIUTUMIA MGAHAWA WA FRESH COACH KUTAPELI..!
Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20.
Mama akilia kwa uchungu.. Keleuwieeeeeee...!!!!!

KANISA LAHIMIZA WAUMINI WAKE KWENDA IBADANI WAKIWA UCHI
KANISA moja nchini Amerika limewaruhusu waumini wake kuhudhuria ibada kanisani huku wakiwa uchi.
Waumini wa kanisa hilo lililoko kusini mwa jimbo la Virginia, sasa wanalazimika kuvua nguo zao pindi tu wanapoingia ndani ya jumba la ibada.
Akihutubia wanahabari, kasisi wa kanisa hilo, Bw Allen Parker, alisema walifikia uamuzi huo wa kuomba uchi baada ya kubainisha kuwa mavazi yana 'udanganyifu fulani’ na akaongezea kwamba hatua hiyo 'itawafanya waumini wote kuwa sawa bila kuwepo kwa utofauti wa kimapato’.
Kasisi huyo alisema hatua hiyo ina ithibati ndani ya Biblia huku akidai kuwa miujiza mingi katika Biblia ilitendeka wakati ambapo wahusika walikuwa uchi. Kwa mfano, alisema Yesu Kristo alikuwa uchi aliposulubishwa msalabani na wakati alifufuka kutoka kaburini.
J
apo matakwa ya kuwa uchi ndani ya kanisa si lazima, wengi wa waumini wanaonekana kuitikia wito huo. Baadhi ya waumini ambao hawapendi kusalia uchi wa mnyama kanisani wanavalia nguo za ndani.
Ambao wamekumbatia wito huo wanasema wamezoea kuwa uchi kanisani japo walikuwa wakiona haya siku za mwanzoni.
Pasta wa kanisa hilo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha runinga nchini humo, alisema anafuata nyayo za Yesu.
“Wakati ambapo Yesu alipitia hatua muhimu maishani alikuwa uchi,” akadai Bw Parker. “Alipozaliwa alikuwa uchi, aliposulubishwa alikuwa uchi na wakati ambapo alifufuka aliacha mavazi yake ndani ya kaburi. Ikiwa Mungu alituumba hivyo, Je, kuna hatia gani kuwa uchi kanisani?” akasaili.
Baridi
Mamia ya waumini wamekuwa wakivumilia baridi ya msimu wa baridi kali kila siku ya Jumapili kusikiliza Injili huku wakiwa uchi wa mnyama.
Wakati huo huo, maelfu ya watu wamekuwa wakifurika kwenye kanisa hilo kupiga picha. Zaidi ya watu 10,000 huzuru kanisa hilo kila mwaka.
“Waumini wanapata fursa ya kusikiliza na kujadili Neno la Mungu,” akasema msimamizi wa kanisa hilo huku akiongezea kuwa kuna baadhi ya watu ambao wana mali nyingi huku wengine hawana kitu chochote.
Alieleza kuwa wanapoomba wakiwa uchi tajiri na maskini huwa sawa mbele ya Mungu.
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE ATINGA MAHAKAMANI
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi hapo jana ametolea ushahidi mbele ya mahakama ya Wilaya ya Njombe dhidi ya kesi ya manunuzi hewa wa magurudumu matano na betri mbili za gari vyoti vikiwa na thamani ya shilingi milioni 14 inayomkabili aliyekuwa kaimu katibutawala wa wilaya hiyo ya wanging'ombe bw Eegray keiya.Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo , mkuu huyo wa Wilaya ya Wanging'ombe ambaye ni shahidi namba moja ameiambia mahakama kuwa ofisi yake pamoja na aliyekuwa akikaimu ofisi ya katibu tawalaWilaya ya Wanging'ombe waliagiziwa magurudumu tano aina ya gunrubk wa ajili ya gari yake lakini hakuwahi kuyaona magurudumu hayokatika ofisi yake."Kwa kipindi kile yanaletwa...
Jumatano, 19 Februari 2014
TAZAMA JINSI MWANAMKE HUYU YALIYOMPATA BAADA YAKUTAKA KUONGEZA UKUBWA WA MAKALIO YAKE
UKRAINE INAWAKA MOTOOOOOOO...!!!

Upinzani huko Ukrain umeapa kutotoka uwanja wa uhuru wanakoendeleza maandamano hayo.
Wakuu kutoka umoja wa Ulaya wameshtumu vikali rais wa Ukrain Viktor Yanukovych, kwa makabiliano makali baina ya polisi na waandamanaji yanayoingia siku ya pili sasa .
Waziiri Mkuu wa Poland , Donald Tusk, amesema atapendekeza Ukrain iwekewe vikwazo vya kiuchumi huku yule wa Sweden Carl Bildt akiongeza kuwa damu ya watu 25 waliokufa katika maandamano hayo iko mikononi mwa Yanukovych.
Vile vile wameutaka upinzani kuzuia machafuko zaidi ambayo yanasambaa kwengineko nchini humo.

IMANI ZA KISHIRIKINA ZAPELEKEA NYUMBA ISHIRINI KUCHOMWA MOTO GEITA
Wananchi wenye hasira kali wameteketeza kwa moto zaidi ya nyumba ishirini na kuvunja nyingine katika kijiji cha Kilombero mkoani Geita kutokana na mauaji ya watu watano yaliyotekelezwa kwa nyakati tofauti kwa kukatwa mapanga. Tukio la Februari 6 la mwanamke Felista Mathias kuuawa kwa mapanga limewachochea zaidi wananchi hao kuvamia nyumba za wanaodaiwa kuhusika februari 17 wakati ukoo ya Kisumo ukitajwa kuhusika na mauaji yanayotokea kijijini humo ambapo mmoja wao Elias Kisumo amekamatwa. Kumekuwa na matukio ya mauaji ya mapanga kwa wazee katika kijiji hiki, na matukio hayo yanahusisha ushirikina, uvamizi wa mifugo katika mashamba ya watu na hata visasi. kuuwawa kwa mwanamke FELISTA MATHIAS mwenye umri wa miaka 55 sababu kubwa...
WAZIRI MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MABWEPANDE
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za Serikali zipatazo 851 zilizopo katika eneo la Mabwepande, Kinondoni,jijini Dar es Salaam zinazosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Huu ni muendelezo na mikakati ya Wizara ya Ujenzi ya kuwajengea na kuwauzia watumishi wa Serikali nyumba kwa bei nafuu.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka Bw. Mwakalinga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Magufuli akiendelea na ukaguzi wa Ujenzi huo.
Hizi ni baadhi ya sehemu ya nyumba hizo.

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)