Ijumaa, 28 Februari 2014
MAISHAPLUS YATINGA KIJIJI CHA IGULA, MCHAKATO KUWAPATA WASHINDI TISA ... 2014
Washiriki 20 wa Maishaplus 2014 wakiwa katika Kijiji cha Igula kata ya Kihologota Tarafa ya Isimani
Washiriki wa Maishaplus wakiangalia kazi yao waliyoifanya ya Ujenzi wa Nyumba iliyobomoka ya Bw. Benad Mfwala katika kijiji cha Igula Kata ya Kihologota Tarafa ya Isimani Mkoani Iringa.
Washiriki wa Maishaplus wakiendelea na kazi za kijamii za ujenzi wa nyumba katika kijiji hicho cha Igula
Washiriki wa maishaplus wakiendelea na kazi ya kuchimba msingi wa choo cha shule ya msingi ya Igula iliyopo kata ya Kihologota Tarafa ya Isimani Mkoani Iringa.
Ni choo cha shule ya msingi ya Igula ambacho washiriki wa maishaplus hao wameweza kukiweka choo hicho taika hali ya usafi kutofautisha na hali ya mwanzo katika choo hicho
Maishaplus 2014 yatinga katika Kijiji cha Igula Kata ya Kihologota kilichopo Tarafa ya Isimani Mkoani Iringa katika mchakato wa kuwapata watu 9 kati ya washiriki 20 waliyoshiriki katika mchezo huo ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia shilingi milioni 25Tsh. Kauli mbiu ya Maishaplus ya mwaka 2014 Ni "REKEBISHA", kwa lengo la kuwataka vijana kubadilika kwa kurekebika katika maisha yao na kuwa na mawazo chanya yenye maendeleo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni