mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Nyama ya swala aliyeuawa na majangili ikiwa kwenye gari. |
Licha ya serikali, wadau pamoja na wahisani wa mali ya asili kuongeza nguvu katika ulinzi, kutoa elimu na kuweka sheria kali za kuwabana majangili ili kukomesha mauaji ya wanyamapori, bado kuna watu wachache ambao mpaka sasa wanavamia hifadhi hizo, wanawinda na kufanya mauaji ya wanayamapori ambapo ni kinyume na sheria.
Usiku wa kuamkia Jumatatu ya tarehe Aprili 20 mwaka huu, vijana kutoka Chuo cha Pasiansi kilichopo Serengeti kwa kushirikiana Kampuni ya Grumeti, walifanikiwa kukamata majangili watatu wakiwa na nyama ya swala aliyenaswa kwenye hifadhi ya Serengeti.
Baada ya kukamatwa, majangili hao walipandishwa kwenye gari la polisi na kupelekwa kituo cha Polisi cha Bunda.
Hii ni oparesheni endelevu katika Hifadhi ya Seregenti ambapo kila wiki majangili kadhaa wanakamatwa na kufikishwa mahakama maalum ya majangili kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni