mcharoman blog fahar yako mtanzania
James Mbatia.
Jimbo la Vunjo: Mgombea wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa kura 60,187 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Innocent Melleck Shirima aliyeambulia kura 16,097.
Nape Nnauye.
Jimbo la Mtama: Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama kupitia CCM, Nape Nnauye ameibuka mshindi katika jimbo hilo. Nape ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa CHADEMA, aliyepata kura 13918.
Jimbo la Ubungo: Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea ameshinda ubunge wa jimbo hilo akimwangusha mpinzani wake Dk. Didas Masaburi wa CCM.
Jimbo la Kigamboni: Mgombea ubunge Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile (CCM) ameshinda ubunge wa jimbo hilo na kufanikiwa kutetea kiti chake.
Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480
Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614.
Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702
Jimbo la Ismani: Wiliiam Lukuvi ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534
Jimbo la Ndanda: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215
Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347
Jimbo la Same Mashariki: Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa kupata kura 18836, dhidi ya kura 15539 za Anne.
Jimbo la Mbogwe: Augustino Manyanda wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 32921, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Maganga Nicodemas Henry wa Chadema, aliyepata kura 13975
Jimbo la Mtwara Mjini: Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa kukitetea kiti chake
Jimbo la Hai: Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966.
Jimbo la Ngara: Alex Gashaza wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 53387, dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Dkt.Peter Bujari wa Chadema aliyepata kura 35254
Zitto Kabwe.
Jimbo la Kigoma Mjini: Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 31546, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Amani Kaburou wa CCM, aliyepata kura 16344
Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12580
Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578
Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649
Jimbo la Njombe Kaskazini: Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.
Jimbo la Dodoma Mjini: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini.
Jimbo la Bukombe: Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe.
Jimbo la Kondoa Mjini: Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini.
Jimbo la Chato: Dk Medad Kalemani Jimbo la Chato (CCM) ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 78817 dhidi ya mpinzani wake Benedicto Lukanima (Chadema) akipata kura 32513.
Jimbo la Bukoba Mjini: Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia Chadema, Wilfred Lwakatale ameibuka mshindi katika jimbo hilo kwa kumshinda mpinzani wake Khamis Kagasheki.
Joseph Mbilinyi (Sugu).
Jimbo la Mbeya Mjini: Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894
Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665
Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183.
Jimbo la Lupembe: Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407
Jimbo la Kasulu Mjini: Mgombea ubunge jimbo la Kasulu Mjini kupitia chama cha CCM, Daniel Sanze ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana huku akimbwaga mpinzani wake Moses Machali wa ACT Wazalendo aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo. Moses Machali amepata kura 22,512 wakati Daniel wa CCM amepata kura 25,336.
Jimbo la Kahama Mjini: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba (CCM), ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana.
Jimbo la Monduli: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli (CHADEMA), Julius Kalenga ametangazwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Hussein Bashe.
Jimbo la Nzega Mjini: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Jimbo la Ilemela: Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (CCM) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo kwa kumbwaga mpinzani wake aliyekuwa mbunge ya jimbo hilo, Highness Kiwia (Chadema). Tarifa zaidi zinasema Kiwia hakuwepo wakati wa kutangazwa matokeo hayo.
Jimbo la Moshi Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, Japhary Raphael Michael (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo kwa kupata jumla ya kura 51656 na kumuangusha Davis Mosha wa CCM.
Jimbo la Bunda Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo na kumuangusha Steven Wasira.
Jimbo la Siha: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Dk. Godwin Mollel,
ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo.
ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Arumeru Mashariki: Joshua Nassari wa Chadema ameshinda ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki akipata kura 86694.
Ester Matiku.
Tarime Mjini: Ester Matiku wa Chadema ameshinda ubunge Jimbo la Tarime Mjini akipata kura 20,017,
Michael Kembati CCM akipata kura 14,025 na Deogratius wa ACT kura 336.
Michael Kembati CCM akipata kura 14,025 na Deogratius wa ACT kura 336.
Lindi Mjini: Hassan Suleiman Kaunje (CCM) ametangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Manispaa ya Lindi, kuwa
Mbunge Mteule wa Jimbo la Lindi Mjini.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Lindi Mjini.
Mbinga Vijijini: Mgombea Martin Msuha (CCM) ametangazwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi, Venance
Mwamengo kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Vijijini baada ya kupata kura 59,269.
Mwamengo kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Vijijini baada ya kupata kura 59,269.
Sixtus Mapunda.
Mbinga Mjini: Mgombea Sixtus Mapunda (CCM), ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Mjini akipata kura 28,324.
Tunduma: Mgombea Mwakajoka Frank (Chadema) ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la
Tunduma (Mbeya) akipata kura 32,442. Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Halima Mpita.
Tunduma (Mbeya) akipata kura 32,442. Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Halima Mpita.
Tandahimba: Mgombea Ubunge wa CUF katika Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Ahmed Katani ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Musoma Mjini: Mgombea Vedatus Mathayo (CCM) ametangazwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Musoma Mjini baada ya kupata kura 32,836
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni