promotion

Jumapili, 27 Septemba 2015

Samia Suluhu aahidi neema kwa wanawake

mcharoman blogy fahar yako mtanzania


Mgombea Mwenza wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Hassan Suluhu, ameahidi kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na kuwawezesha kiuchumi kupitia sera zenye kutoa fursa.

Suluhu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati alihutubia kongamano la wanawake wa vyuo vikuu na wanataaluma. 

Alisema kuwa wanawake ni nguzo kubwa katika taifa hivyo changamoto zinazowakabili zikitatuliwa taifa litakua kimaendeleo. 

Fursa hizi ni kumuwezesha kiuchumi katika kuwafungulia sera zenye fursa mbalimbali ambazo zitamfanya mwanamke kusonga  mbele katika kujiongezea uchumi, alisema.

Suluhu alisema anatambua moja ya vikwazo ni barabara na tayari suala hilo linashughulikiwa ili waweze kufanya shughuli zao bila kuwapo na matatizo.

Alisema anaelewa changamoto ya umeme katika baadhi ya maeneo hivyo Chama Cha Mapinduzi kikiingia tena madarakani kitahakikisha katika kipindi cha miaka miwili umeme unapatikana nchi nzima. 

Aidha, alisema viwanda vitaanzishwa katika maeneo ya vijijini ili kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima na asilimia 40 ya ajira zitatokana na kilimo.

Suluhu alisema anatambua mfumo wa  stakabadhi ghalani kwa sasa una matatizo hivyo suala hilo litasimamiwa ili kuhakikisha wakulima wanafaidika kupitia mfumo huo.

Hata hivyo, alisema kuna fedha ambazo hutakiwa kutengwa katika halmashauri kiasi cha asimilia 10 ya mapato ambacho hutakiwa kupewa wanawake na vijana.

Aliahidi kulisimamia ili fedha hizo ziwafikie walengwa.
Aidha, alisema kwenye afya kuna changamoto nyingi  kwani vijiji vingi havina zahanati, kukosekana kwa dawa, watumishi wachache pamoja na vifaa.

Alisema kwa upande wa dawa, alisema watafuatilia kwa njia ya mtandao kuanzia zinakotoka hadi zinapofikia kwenye Bohari ya Dawa (MSD) na zinapotolewa kuelekea vituo vya afya lengo ni kukomesha wizi.

Suluhu alisema CCM inatambua tatizo la vifo wa akina mama hasa wakati wa kujifungua na kuahidi kuwa suala hilo litashughulikiwa kikamilifu kwani vingine husababishwa na ukosefu wa vifaa pamoja na wataalamu. 

Alisema vyuo ambavyo vinafundisha wataalam hao vimekuwa vikiendesha elimu hiyo kwa gharama kubwa, hivyo wanajipanga kutoa vyuo vya serikali kuvipeleka kwenye sekta binafsi ili kutoa mafunzo hayo kwa bei powa.

Hata hivyo, katika kongamano hilo wataalam mbalimbali walitoa mada zao huku wakilalamikia wanawake kutopewa fursa ya kumiliki rasilimali, kukosekana kwa vitendea kazi kwa walimu, wanafunzi kusoma katika mazingira magumu, kukosekana kwa sera zinazomuwezesha mwanamke kusafirisha bidhaa zake na tatizo la vifo vya akina mama wakati wa kujifungua.

Hakuna maoni: