mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Simanzi na vilio vilitawala wakati mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana.
Mume wa marehemu, Swaleh Pongolani, aliangua kilio na kuongeza huzuni kubwa kwa watu mbalimbali waliokuwapo uwanjani hapo kuupokea mwili wa marehemu wakiwamo viongozi mbalimbali wa serikali, wanafamilia, wafanyakazi wa wizara yake na wa ofisi ya bunge.
Wakiongozwa na Mama Salma Kikwete, Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Mgombea mweza wa nafasi ya urais CCM, Samia Suluhu, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Ramadhan Kailima na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila wote walijawa na huzuni kubwa.
Wengine ni mawaziri, wabunge, viongozi wa chama, ndugu na marafiki.
Mwili huo ulipokelewa saa 9:40 alasiri na askari wa bunge na kuingizwa moja kwa moja kwenye gari la wagongwa (ambulance) na kisha kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake, Mikocheni jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Akizungumzia hatima ya uchaguzi katika Jimbo la Ulanga Mashariki ambalo Kombani alikuwa anagombea kupitia CCM, Mkurugenzi wa Nec, Kailima, alisema utaahirishwa.
Alifafanua kuwa baada ya uchaguzi mkuu kumalizika, CCM itapewa siku 30 kumteua mgombea mwingine kugombea nafasi hiyo na kwamba taarifa nyingine zitaendelewa kutolewa.
Kombani alifariki Alhamisi wiki hii nchini India alipokuwa anatibiwa, na anatarajiwa kuzikwa wiki ijayo mkoani Morogoro.

CHANZO: NIPASHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni