mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Henry Shekifu |
Wabunge wa bunge la vijana Wilaya ya Lushoto, wametangaza mgogoro na wabunge wa majimbo ya Lushoto, Henry Shekifu na January Makamba wa Bumbuli kwamba wameshindwa kuwa kivutio cha maendeleo kwa wananchi wao.
Tamko hilo lilitolewa jana na Spika wa bunge hilo, Frank Shempemba, katika kikao cha bunge kilichofanyika ukumbi wa vijana uliyopo kijiji cha Mbelei jimbo la Bumbuli wilayani hapa.
Shempemba ambaye pia ni Spika wa bunge la vijana la Mkoa wa Tanga na
mjumbe wa UVCCM Wilaya ya Lushoto, alisema wabunge hao hawakuwa kivutio cha maendeleo na badala yake wametanguliza ubinafsi na kuwagawa wapigakura.
Tamko hilo limekuja baada ya wabunge hao wa vijana kueleza changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wao kwa jamii na wabunge wa majimbo hayo kutajwa kuwa miongoni mwa vikwazo.
"Makamba ambaye ni Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia, atakumbukwa kwa kufunga kiwanda cha chai Mponde na kuwaachia umasikini wakulima na kuwagawa kisiasa wananchi," alisema.
Awali akichangia mjadala wa jinsi ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma na uwajibikaji kijamii, Mbunge wa Kata ya Kwemashai, James Mponda, alielezea mradi wa maji wa Ngumshi ambao umekwamishwa na Shekifu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga kutokana na ubinafsi.
Mponda alisema kuwa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.6 umepokea Sh. milioni 500. 3 kati ya hizo na wahisani fedha ambazo Shekifu anadaiwa kuzizuia na kuusimamisha kama shinikizo la kutaka wananchi wamchague tena katika uchaguzi mkuu ujao.
“Tulimfuata kama wabunge wa vijana kutaka kujua sababu ya kusimamishwa mradi huo, akatamka kama tunataka maji tuhakikishe anapita kura za maoni na kumchagua tena si vinginevyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeomba fedha hizo Benki ya Dunia” alisema Mponda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni