Mkuu
wa wilaya ya bariadi na pia kaimu mkuu wa wilaya ya maswa mkoani simiyu
Mh. Ponsiano Damiano Nyami akiwa ndani ya studio za redio sibuka fm
Tatizo la mauaji ya watu waishio na ulemavu wa ngozi (Albinism) limekuwa kubwa hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni simiyu,shinyanga,mwanza na mingine ambayo ipo ukanda huu ambapo sababu kubwa ni uelewa mdogo wa watu wanaofanya vitendo hivyo
Akizungumzia suala hilo mkuu wa mkoa wa bariadi mkoani simiyu ambaye pia anakaimu kwa wilaya ya maswa katika kipindi cha pambazuko la afrika mashariki kinachorushwa na redio sibuka fm amesema suala hili linatakiwa kila mmoja kwanza awe na hofu ya mungu kwa kutomtendea mwenzake kitu kibaya ambacho yeye mwenyewe hapendi atendewe "Kila mtu anasiku yake ya kufa na pia siku hii ya kufa ndiyo siku ya mwisho kwake kuishi hapa duniani kwa hiyo ni vizuri kumuogopa mungu kwan yeye ndiye anayepanga kila kitu na sio binadamu na pia mungu ndiye aliyetuumba sisi sote iweje wewe umuue mwenzako" Alihoji mkuu huyo
Mh.Ponsiano Nyami akisisitizia jambo flani akiwa studioni |
Kwaupande mwingine amewahimiza wananchi katika suala la kujenga maabara katika shule za sekondary nchini ili kuweza kuapata wataalamu wa masuala mbalimbali baada ya kupata elimu kupitia maabara hizo
Pamoja na hayo pia kuhusu suala la chanjo kwa watoto wenye umri kati ta miaka mitano hadi kumi na nne amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto hao katika shule mbali mbali kuweza kupata chanjo hiyo ambayo inatolewa kuanzia tarehe 21/05/2015 hadi 22/05/2015 kwa wilaya ya maswa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni