promotion

Alhamisi, 21 Mei 2015

IDADI YA WAGONJWA WALIOGUA UGONJWA WA AJABU SIMIYU YAONGEZEKA NAKUFIKIA ELFU MOJA (1000.)

mcharoman blogy fahar yako mtanzania

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu eraston Mbwilo akiongea na wananchi katika wilaya ya Meatu.


Idadi ya wagonja ambao wameugua ugunjwa wa ajabu uliozikumba jumla ya kata 6 katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu imezidi kuongezeka kila mara, tangu kuripotiwa kutokea kwa ugonjwa huo wiki mbili zilizopita.

Mpaka jana taarifa zilizotolewa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Meatu Adamu Jimisha alisema kuwa idadi hiyo imeongezeka kutoka wagonjwa 80 hadi kufikia 1048 ambao walifikishwa katika kituo cha afya Mwandoya.

Jimishi alitoa taarifa hiyo jana mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, iliyokuwa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Elaston Mbwilo, wakati ilipowatembelea baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika kituo hicho cha afya pamoja na kata za, Mwabusalu, Lingeka, Mwakisandu, Tindabuligi, Pamoja na Lubiga ambazo zimekubwa na janga hilo.

Alieleza kuwa bado dalili za baadhi ya wagonjwa ambao wamekuwa waliletwa katika kituo hicho cha afya tangu kutokea kwake, zimekuwa ni zilezile kumwa kichwa, kikohozi kikavu, mwili kulegea, kuchanganyikiwa akili pamoja na kupoteza fahamu.

Aidha aliongeza kuwa wagonjwa hao wamekuwa wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani pindi wanapopata nafuu au kupona kabisa, huku akibainisha kuwa baadhi yao walikutwa na magonjwa mbalimbali kama maralia na minyoo.

Mganga Mkuu huyo alieleza kuwa wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiambatana na Timu ya Mkoa akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa, Mtaalam wa Maabara na Daktari mmoja walichukua sampuli kwa ajili ya kupeleka Nairobi kwa Uchunguzi.

Alisema timu hiyo ilipeleka vipimo hivyo tarehe 15/05/2015 kwa ajili ya kubaini aina gani ya ugonjwa, ambapo majibu alieleza kuwa timu hiyo iliahidi kutoa mwishoni mwa mwezi huu.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo waliokuwa wamefika kuwajulia hali baadhi ya wagonjwa katika kutoa hicho cha afya kuwapeleka mapema hospitali watu watakaoonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.

 wa binadamu usiojulikana ambao uliripotiwa mapema mwezi Mei na kuathiri Tarafa ya Kisesa na baadhi ya maeneo ya Tarafa ya Kimali, wilayani Meatu.

Mhe. Mbwilo aliyasema hayo jana wakati alipozungumza na wananchi mara baada ya kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika Kituo cha Afya cha Mwandoya.

Mhe. Mbwilo alisema kuwa kutokana na taarifa aliyoipokea kutoka kwa Daktari Msaidizi wa Kituo hicho cha afya inaonesha kuwa wagonjwa wanaopelekwa mapema hospitali na kupatiwa matibabu wanapata nafuu mapema kuliko wale waliocheleweshwa.

“ Msiiwaache wagonjwa majumbani waleteni na msiwapeleke kwa waganga wa kienyeji,  mkiona watu wenye dalili za ugonjwa kama walivyowaeleza wataalam waleteni haraka hapa Mwandoya wapatiwe matibabu” alisema Mbwilo.

Mbwilo aliwaeleza wananchi kuwa kwa mujibu wa Watalaam wa Afya ugonjwa huo hauna madhara ya kifo, hivyo akawataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida wakati Serikali inaendelea kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha ugonjwa huo.

Nao baadhi ya wananchi wakiongea mbele ya mkuu huyo wa Mkoa waliiomba Serikali kufuatilia haraka matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa na Wataalam hao ili wajue chanzo cha ugonjwa huo ambao mpaka sasa hawaujajulikana.

 “Tunaomba majibu ya vipimo vilivyochukuliwa yaletwe haraka, maana mpaka sasa hivi hatujui huu ni ugonjwa gani na chanzo chake nini, Serikali itusaidie katika hili” alisema mmoja wa wananchi alijulikana kwa jina la Joseph.

Mhe Mbwilo alisema Serikali inaendelea kufuatilia majibu ya vipimo hivyo vilivyochukuliwa na Timu ya Wataalam wa Afya  kutoka Mkoa wa Simiyu na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  baada ya kukamilisha taarifa zitatolewa kwa wananchi.


            SOURCE SIMIYU NEWZ

Hakuna maoni: