promotion

Jumatatu, 20 Aprili 2015

WAUGUZI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MASWA MKOANI SIMIYU WAMKATAA MGANGA MFAWIDHI WA HOSPITALI HIYO

mcharoman blogy fahar yako mtanzania



WAGANGA na Wauguzi katika hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu
wamemkataa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ,Dr Albert Mnyanzila kwa
madai kuwa amekuwa akitumia ubabe pamoja na lugha chafu kwa wafanyakazi hao.

Watumishi hao mbali na kupaza sauti zao kumkataa kiongozi huyo, wamemtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Trasiasi Kagenzi pamoja na Mganga Mkuu wa wilaya Dr Jonathan Budenu kumwondoa mara moja Dr Mnyanzila katika nafasi hiyo.

wakiongea na waandishi wa habari hospitalini hapo watumishi hao walieleza kuwa kiongozi wao hana  sifa za kuongoza watumishi wanaohudumia wagonjwa katika hospitali hiyo kutokana na kukosa hekima pamoja na busara za kiongozi katika kuongoza watu waliochini yake.

Walisema kuwa kutokana na tabia yake ya ubabe na lugha chafu kwa
watumishi wenzake hali ambayo imesababisha kuwepo kwa migomo baridi ya
Madaktari,Waganga na Wauguzi jambo ambalo limefanya wagonjwa kutopata
huduma kwa wakati muafaka.

 watumishi hao walienda mbele zaidi na kueleza kuwa Kiongozi huyo amekuwa chanzo cha migogoro mingi isiyoisha kati ya uongozi wa hospitali na wafanyakazi huku wakitahadharisha iwapo halmashauri ya wilaya haitachukua hatua dhidi ya Dr Mnyanzilwa watatangaza mgomo usiokuwa na kikomo wa kutotoa huduma kwa wagonjwa.

Alipotafutwa na na Simiyu News kujibu tuhuma zinazomkabili Dr Mnyanzila alikataa kusema lolote na kuwashukuru waandishi wa habari kwa kupata habari hizo na kuwataka kumwona Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa kwani ndiye Mwajiri wake.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa,Vivian Chirstian
akizungumzia malalamiko hayo alisema kuwa suala hilo tayari limefika
ofisini kwake na atalishughulikia  haraka ipasavyo ili kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora katika  Hospitali hiyo ya Wilaya.

Hakuna maoni: