promotion

Alhamisi, 23 Aprili 2015

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASWA MKOANI SIMIYU NDG. TRANSIAN KAGENZ AMEKANUSHA VIKALI SUALA LA MGANGA MFAWIDHI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MASWA KUKATALIWA NA WAUGUZI

mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya maswa Ndg Transias Kagenz
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya maswa mkoani simiyu Ng transias kagenzi amekanusha suala lamganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya maswa Dr Albert Mnyanzila  
kukataliwa na wauguzi wa hospitali hiyo na kusema kuwa ni uzushi pia hakuna ukweli ndani yake 

Kwa mujibu wa taarifa za awali zilidai kuwa wauguzi katika hospitali hiyo walikataa uongozi wake kutokana na lugha chafu pamoja na uongozi wa kibabe katika hospitali hiyo 

wakiongea na waandishi wa habari hospitalini hapo watumishi hao walieleza kuwa kiongozi wao hana  sifa za kuongoza watumishi wanaohudumia wagonjwa katika hospitali hiyo kutokana na kukosa hekima pamoja na busara za kiongozi katika kuongoza watu waliochini yake.

Walisema kuwa kutokana na tabia yake ya ubabe na lugha chafu kwa
watumishi wenzake hali ambayo imesababisha kuwepo kwa migomo baridi ya
Madaktari,Waganga na Wauguzi jambo ambalo limefanya wagonjwa kutopata
huduma kwa wakati muafaka.

 pamoja na hayo kwa upande wake Dr Albert alidai kuwa hakuna kauli mbaya yeyote anayoitumia katika uongozi wake Hata hivyo alisema yeye kama kiongozi anafanya kazi kulingana na sheria inavyomruhusu 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa,Vivian Chirstian
Mara baada ya kuzungumza na Mcharoman blogy alisema kuwa suala hilo tayari limefika ofisini kwake na analishughulikia  haraka ipasavyo ili kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora katika  Hospitali hiyo ya Wilaya.

Hakuna maoni: