promotion

Jumanne, 24 Machi 2015

Rais Kikwete amesema atahakikisha anatimiza ahadi alizozitoa kabla ya kumaliza muda wake

mcharoman blogy fahar yako mtanzania


Rais Jakaya Kikwete amesema atahakikisha kablaya ya kumaliza muda wake wa uongozi anatimiza ahadi alizozitoa ili kumpungumzia kazi rais ajaye na kuongeza kama kutakuwa kuna mambo yamebaki atayakabidhi  kwa mrithi wake hivyo wananchi wasiwe na wasi wasi.

Mh Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha mafunzo ya maafisa wa Polisi ambapo amewagiza kuhakisha kuwa mauaji ya  Alibino yanakoma.

Aidha Mh rais amelitaka jeshi hilo la polisi kuhakisha inajiepusha na vitendo vya rushwa kwani vinalichafua pamoja na kuongeza nguvu kupambana matukio ya ugadi ambayo kwa sasa yameanza kushamiri nchini.
 
Kwa upande wake naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Pereira Silima amewataka polisi kwakuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na hivyo lazima wafanye mambo kwa utafiti.
Ernest Mangu ni mkuu wa jeshi la Polisi nchini ambaye katika hotuba yake amesema nchi bado ipo salama sana ukilinganisha na nchi jirani ambapo mkuu wa chuo cha  taaluma ya Polisi katika amesema waliohitimu ni askari 290 huku wanafunzi saba wakishindwa kumaliza kutokana na sababu mbalimbali ikwemo utovu wa nidhamu