promotion

Jumapili, 1 Machi 2015

MAREHEMU JOHN KOMBA AACHA MKE WA NA WATOTO 11 TUTAKUENZI KWA YALE MEMA ULIOKUWA UNAONYESHA KWA TAIFA LAKO



Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia jana alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .
 

Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.

Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni jana akiwa mahututi .

"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk Ishan

Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.
 
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.
mcharoman blogy

Hakuna maoni: