mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh;Jakaya Mrisho Kikwete |
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya
Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York wakati wa ufunguzi wa Mkutano
unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye
utu (Achieving sustainable development through employment creation and
decent work).
Rais
Kikwete amesema tatizo la ajira lina pande mbili, kwanza linaweza kutumika
vizuri pale wawekezaji wanapokuja barani Afrika, wanaweza kupata
nguvu kazi iliyopo tayari, ikiwa inakidhi matakwa ya kazi na pili ni
changamoto kubwa pale ambapo ajira hazipatikani kwa kundi kubwa la vijana ambao
wanaongezeka kila mwaka.
"Hivyo
ni muhimu ukuzaji wa ajira kuwa kipengele muhimu katika ajenda ya maendeleo,
mipango na programu mbalimbali katika Mataifa yote"
Rais amesema na kuelezea kuwa pamoja na ukweli uliopo kuwa nchi mbalimbali
barani Afrika ikiwemo Tanzania, zimeonyesha hali nzuri ya uchumi kwa miongo
miwili mpaka mitatu iliyopita, na kuonyesha kuwa bara la Afrika ni moja ya mabara
yanayokua kwa kasi kiuchumi duniani, bado bara linakabiliwa na tatizo kubwa la
ajira.
"Natarajia
tutabadilishana mawazo ya jinsi gani Afrika inaweza kutatua tatizo hili na pia
kupata mawazo ya nini kifanyike kuweza kuvutia wawekezaji zaidi". Rais
amesema.
"Pia
nitapenda kupata mawazo na ikiwezekana kuunga mkono katika kusaidia vijana wetu
katika suala la kujiajiri" ameongeza na kusema
suala hili linahitaji programu maalum na miradi.
Rais
Kikwete amezungumzia suala la ajira barani Afrika kuwa la kutia mashaka na
hivyo kuhitaji hatua za haraka. Takwimu zinaonesha kuwa Afrika ilitengeneza
ajira 37 million pekee kwa kipindi cha
muongo uliopita, kati ya hizi asilimia 28 zilikuwa ajira zenye utu, na wakati
huo huo inakadiriwa kuwa, soko la ajira barani Afrika linapokea watu milioni
122 katika ajira mpya kila mwaka.
"Hii
inatisha sana kwa vile karibu watu 200 barani Afrika ni wake wenye miaka 15 na
24 na kwamba idadi hii itaongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2045"
Rais amefafanua na
kuonyesha wasiwasi wake kwamba bara la Afrika litakumbwa na idadi kubwa ya
ukosefu wa ajira, na kibaya zaidi idadi kubwa kuwa ya vijana.
.............Mwisho.............
.............Mwisho.............
Imetolewa na;
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi,
New York - USA
31 Aprili, 2015
New York - USA
31 Aprili, 2015