promotion

Jumanne, 31 Machi 2015

ASKARI MAGEREZA ALIYEKAMATWA NA NOTI BANDIA SIMIYU ATIMULIWA KAZI RASMI.

                    mcharoman blogy fahar yako mtanzania

Edmund Masaga ambaye alikuwa askari magereza katika gereza la wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ambaye jana amefukuzwa kazi kwa kile kilichodaiwa kukutwa naoti Bandia.






Naibu kamishna wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu Charles Mkumbo akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya sare za fedha bandia ambazo zilikamatwa askari wa jeshi la polisi Mkoani hapa pamoja na Askari Magereza wilayani Bariadi


Jeshi la Magereza nchini limemfukuza kazi askari wake wa Gereza Bariadi, Mkoani Simiyu kwa kosa la kupatikana na fadha za bandia kinyume na Sheria za Nchi.
 
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana wa jeshi hilo nchini Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja, askari Na. B. 6499 Wdr. Edmund Masaga amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28, 2015 kwa kosa la kulidhalilisha Jeshi mbele ya Umma kinyume na Kanuni 22(xlix) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Magereza za Mwaka 1997.
 
Aidha, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amekemea vikali vitendo hivyo kwani ni kinyume cha Maadili na Utendaji ndani ya Jeshi la Magereza huku akiwataka askari wote wa Jeshi la Magereza nchini kutenda kazi zao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

Hata hivyo taarifa kutoka katika jeshi la polisi Mkoani Simiyu zinaleleza kuwa Tayari askari wakemwenye namba H 2420 PC Seleman Juma (25) ambaye ni askari wa kikosi cha kutuliza gasia FFU Mkoani Simiyu Tayari amefukuzwa kazi na ijumaa wiki iliyopita wote wawili walifikishwa mahakamani.