mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Baada ya kutuhumiwa kuwa ndiyo chanzo kikuu katika matukio ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) pamoja na vikongwe kwa imani za kishirikina waganga wa jadi wadaiwa kufanya mapenzi na wateja wao na kuhatarisha ndoa za watu.
Baada ya kutuhumiwa kuwa ndiyo chanzo kikuu katika matukio ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) pamoja na vikongwe kwa imani za kishirikina waganga wa jadi wadaiwa kufanya mapenzi na wateja wao na kuhatarisha ndoa za watu.
Waganga hao wameelezwa kufanya vitendo hivyo pindi wateja wao wanapokwenda kupatiwa huduma ya tiba asili, ambapo wengine wamedai kuwalazimisha kufanya tendo la ndoa pasipo hiari yao (kubakwa).
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Shirika la Maendeleo na Utafiti Tiba asili Tanzania (SHIMAUTITA) Aron Mbeo, wakati wa Mkutano Mkuu wa Shirika hilo kwa wanachama wake wakiwemo waganga wa tiba asili Mkoani Simiyu uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Wilayani Bariadi.
Alisema katika utafiti uliofanywa na shirika hilo ndani ya kata 10 katika Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Katibu huyo alisema kuwa utafiti huo ulibaini kuwepo kwa idadi kubwa ya waganga wa jadi wanaofanya vitendo hivyo kwa wateja wao.
Alisema kuwa wengi wa waganga hao wanaofanya vitendo hivyo wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kuhamahama, ambapo alibanisha kuwa katika utatfiti huo ilibaini kuwa wao ndiyo chanzo kikubwa cha kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na vikongwe.
“ utafiti huu tumeufaya mwaka 2014..na kubaini asilimia kubwa ya waganga wa jadi wanaohamahama wamekuwa wakisababisha ndoa za wateja wao kuvunjika..wanawalazimisha mapenzi..lakini wakikataa utumia dawa hadi kuwapata ..na wengi wao wanawapenda hadi watoto wadogo na walioko shuleni.tabia hii ni kubwa ndani ya Mkoa huu” Alisema Mbeo.
Aliongeza kuwa baadhi ya wateja ambao ukataa kufanya vitendo hivyo wamekuwa wakilazimishwa hadi kubakwa ikiwa pamoja na kutishiwa kuuawa ikiwa watatoa taarifa kuwa wamebakwa na waganga hao.
Mbeo alibainisha kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha wananchi wengi kukosa imani na kazi za waganga hao, huku wengine wakikata tamaa ya kuendelea kutumia dawa ya asili.
Mbali na tuhuma hizo kwa waganga hao, ilielezwa kuwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumika kwenda kuwakata mapanga vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wamekuwa wakioshwa( kusafishwa) na waganga hao ili wasikamatwa au kupata ujasili wa kutenda unyama huo.
Katibu huyo alieleza kuwa hali hiyo imekuwa kisababishi kikuu kwa serikali kufanya msako wa kuwakata waganga wanaopiga ramli chonganishi, lengo likiwa kupunguza hadi kukomesha vitendo vya kuuawa kwa watu hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Dr Machakosi Sinja alieleza kuwa katika utafiti huo ilibainika kuwa asilimia 90 ya waganga wa jadi hawajuhi sheria na taratibu za tiba asilia.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwafanya waganga wengi kufanya kazi zao bila ya kufuata taratibu, ikiwa pamoja na kujihusisha katika ramli chonganishi huku akieleza kuwa wengi wamekuwa wakifanya kazi hizo kwa kujificha.
Alisema shirika hilo kwa hivi sasa limeandaa mkakati mkubwa wa kuweza kupambana na hali hiyo, kutoa elimu kwa waganga hao ikiwa pamoja na kuungana na serikali katika mapambano ya kupiga vita ramli chonganishi.
Hata hivyo mgeni rasmi katika Mkutano huo ambaye alikuwa kaimu Mkuu wa wilaya ya Bariadi Albert Rutahiwa aliwataka wagaga hao kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanasajiliwa kuanzia ngazi za mitaa au vijiji kwa ajili ya kuwapatiwa leseni.