promotion

Ijumaa, 13 Februari 2015

MAMBO MUHIMU YAKUFAHAMU SIKU HII YA VALENTINE'S DAY!!! {kwa wapendanao]

mcharoman blogy

Siku hii inaonekana ni maalumu kwa ajili ya kuonyeshana upendo wa dhati kwa mtu yeyote. Ni siku muhimu na yenye maana kubwa kwa kila mtu, maana upendo hauchagui.
Ingawa wengine wanaweza kuitumia au kuichukulia kwa kadri wanavyotaka, msingi wa siku hii hasa ni kuonyesha upendo kwa watu, si lazima awe mke au mumeo ama mchumba.
Maana na ukweli wa uwepo wa  siku hii inayoitwa Valentine’s Day inaharibiwa na baadhi ya watu kwa kuiona kama ni siku ya kufanya ngono/uzinzi. Ukitaka kuthibitisha hili, siyo lazima uende chuo kikuu ili kupata ujuzi wa kujua ukweli, bali tembelea nyumba za wageni zilizo karibu, nyingi utakutana na bango ‘vyumba vimejaa! Nchini Italia wakati huo kulikuwa na kiongozi aliyeitwa Mfalme Claudius II; aliamini kuwa askari anapooa hawi mkakamavu na pia muda mwingi anawaza kuhusu familia yake zaidi ya kitu kingine chochote. Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.
Kitendo hicho hakikuwafurahisha watu wengi, akiwamo Padri Valentino. Kiongozi huyu wa kidini aliendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentino  akamatwe na kuuawa. Mtakatifu Valentino aliuawa siku na tarehe kama ya leo, ndiyo maana ikatangazwa rasmi kuadhimishwa kwa ajili ya kumkumbuka kama Baba wa Upendo na mtetezi wa wanandoa. Historia zinaonyesha kuwa aliyetangaza rasmi kuadhimisha siku hiyo ni Papa Gelasius.
Aidha, iko simulizi nyingine inayosema kuwa  akiwa gerezani Valentino  aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za Valentino kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa kusema ‘Kutoka kwa Valentino wako’.
Tangu hapo Valentino  anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa ulimwenguni kote’


NAMNA INAVYOPASWA

Msingi hasa wa siku hii ni kuonyesha upendo, hii ina maana kuwa unaweza kuonyesha upendo kwa yeyote iwe ni jirani, mzazi au yeyote unayempenda, siyo lazima mpenzi kama ambavyo baadhi ya watu wanafanya.
Waweza kumtumia ujumbe mzuri mtu yeyote unayempenda au hata zawadi, waweza kutembelea yatima, wagonjwa na hata watu wengine wowote; kubwa hasa kwa siku hii ni kuonyesha upendo.
Hata hivyo, kwa sababu ya ukweli kwamba wengi wanaiona kama ni siku ya ngono, ni suala la msingi sana unapotoa zawadi kwa mtu wa jinsi tofauti kuwa makini; angalia zawadi unayoitoa isije ikaharibu siku yako na maisha yako kwa jumla badala ya kukupa furaha, kwa sababu baadhi ya wenza wa wale ambao unaweza kuwapa zawadi wanaweza kutafsiri kama wewe una uhusiano wa kimapenzi na mtu huyo.


Hakuna maoni: