Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakimhoji binti huyo
ambapo baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary Joseph.
Anasema leo ni mara ya tatu wanakuja kufanya uchawi wao,lengo lao ni kutaka ndugu yao aolewe na Massawe,walikuja siku ya kwanza wakakuta mke wa Massawe akisali,wakashindwa,wakarudi mara ya pili kwa ajili ya kusambaratisha ndoa,wakafanikiwa leo walikuja kufanya sherehe kwa kazi hiyo lakini wenzake wamemkimbia-Picha zote na Kadama Malunde- |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni